Pamoja na sheria mama za nchi, uongozi wa jimbo la Musoma Vijijini unawakumbusha wanachi kuzingatia sheria na kanuni zifuatazo.
- Kila mzazi au mlezi mwenye mtoto aliyefikisha umri wa kuanza shule analazimika kumuandikisha mtoto huyo kuanza shule.
- Kila mwananchi anayejishughulisha na shughuli za uvuvi wa samaki, anapaswa kuzingatia kutotumia au kushiriki kwa namna yoyote ile katika uvuvi haramu.
- Kila kaya inapaswa kuhakikisha kuwa eneo la kaya husika ni safi.