VIJIJI VIWILI VYA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI VYAAMUA KUJENGA SEKONDARI YAO 

Mafundi na Wanavijiji wa Kigera Etuma na Kakisheri wakiendelea na Ujenzi wa Jengo la Utawala la Kigera Secondary School.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Vijiji vya Kigera Etuma na Kakisheri vyote vya Kata ya Nyakatende vimeanza kwa kasi kubwa kujenga Sekondari yao. Sababu kuu za UAMUZI huu ni UMBALI MREFU wa kutembea na MSONGAMANO Madarasani wa Wanafunzi kwenye Sekondari ya Kata iliyoko Kijijini Nyakatende.
Wanavijiji hawa tayari wamekamilisha ujenzi wa Boma la Vyumba viwili vya Madarasa ambavyo vimejengwa kwa kutumia MICHANGO ya WANAVIJIJI na WAZALIWA wa Vijiji hivyo viwili. HARAMBEE ya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo imeongeza kasi ya ujenzi wa Jengo la Utawala.
MTINDO WA KUTOA MICHANGO
Wakazi wa Vijiji vya Kigera Etuma na Kakisheri WAMEKUBALIANA kwamba kila MWANAKIJIJI mwenye umri wa kuanzia MIAKA 18 achangie TOFALI MOJA. Mawe, kokoto, mchanga na maji ya kujengea vinasombwa kwa kutumia NGUVUKAZI  zao.
WADAU wengine wenye kuchangia ujenzi huu ni: WAVUVI na WACHIMBAJI Wadogo Wadogo wanaofanya shughuli zao Vijijini hapo.
Aidha, Katibu wa Kamati ya ujenzi wa Sekondari hiyo Ndugu James Majengo, kwa niaba ya Uongozi na Wananchi wa Vijiji vya Kigera Etuma na Kakisheri, anatoa SHUKRANI nyingi kwa WAZALIWA wa Vijiji vya Kakisheri na Kigera Etuma kwa MICHANGO yao mikubwa.
Vilevile, SHUKRANI nyingi zimetolewa kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo aliyechangia SARUJI MIFUKO 100.
WAZALIWA wa Vijiji vya Kigera Etuma na Kakisheri WAMEUNDA UMOJA WAO kwa ajili ya kuchangia ujenzi huu. Hadi sasa waliochangia ni:
(1) Nyakiriga Kabende-Mwenyekiti
(2) Albinus Makanyaga-Mhasibu
(3)Joseph Mnibhi – Katibu
(4) Augostino Eugene
(5) Joseph Surusi
(6) Wambura Mujungu
(7) Marere Eugene
(8) Mareges Eugene
(9) Emmanuel Ekama
(10) Mareges Jela
(11) Kisha Charamba
(12) Garani Magafu
(13) Mugini Kibusi Marere
(14) Ngajeni Manumbu
(15) Lucas Mashauri
(16) Mutandu Kabende
(17) Boniphace Kitende
(18) Boniphace Changanya
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 na Vijiji 68 lina Sekondari za Kata/Serikali 18 na 2 za Binafsi. Wanavijiji WAMEAMUA kujenga SEKONDARI MPYA NANE (8).