WAZAZI WA KATA YA TEGERUKA WAAGA VIJANA WAO KWA ZAWADI YA KIPEKEE

baadhi ya MATUKIO ya MAHAFALI ya Wanafunzi wa Darasa la VII  wa S/M Nyaminya A&B, Kijijini Tegeruka, Kata ya Tegeruka.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
WAZAZI wa Wanafunzi wa S/M Nyaminya A na B zote za Kijiji cha Tegeruka, Kata ya Tegeruka wamewaaga WATOTO wao watakaohitimu Elimu ya Msingi kwa kutoa ZAWADI ya uchangiaji wa UJENZI na UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya ELIMU katika Shule hizo mbili.
Zoezi hilo limefanyika jana Agosti 23, 2019 kwenye MAHAFALI ya kuwaaga WANAFUNZI wa Darasa la VII wa Shule hizo.
ZAWADI hiyo imetokana na MGENI RASMI, Ndugu SHAIBU NGATICHE, Katibu wa CCM Mkoa wa Mara kupokea Changamoto za Shule ya Msingi Nyaminya B ambazo ziliwasilishwa na Mkuu wa Shule hiyo, Mwl Zerulia John Shana.
Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Upungufu wa Vyumba vya Madarasa. Nyingine ni kutokuwepo SAKAFU kwenye  baadhi ya Vyumba vya Madarasa na upungufu wa Nyumba za kuishi Walimu.
Baada ya kupokea orodha ya Changamoto hizo, MGENI RASMI waliwasihi WAZAZI na WAGENI wengine kwenye MAHAFALI hiyo KUUNGANA nae KUTATUA baadhi ya matatizo hayo.
HARAMBEE ilipigwa na matokeo yake ni:
(1) Saruji  Mifuko: 140
(2) Misumari: Kg 10
(3) Milango ya Vyumba vya Madarasa: 2
(4) Fedha Tsh 2,175,100/=
(5) NGUVUKAZI: Wanavijiji WAMEKUBALI KUJITOLEA kusomba mchanga, mawe, kokoto na maji ya ujenzi.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alichangia SARUJI MIFUKO 100 (kila Shule Mifuko 50) na MILANGO 2 ya Vyumba vya Madarasa (kila Shule Mlango 1 wenye thamani ya Tsh 150,000).
Mara baada ya HARAMBEE hiyo, Mwl Mkuu wa S/M Nyaminya B,  mwenyeji wa Sherehe hizi, Mwl Zerulia John Shana, ALIMSHUKURU SANA MGENI RASMI, Ndugu SHAIBU NGATICHE kwa kuendesha HARAMBEE hiyo iliyokuwa ya MAFANIKIO mazuri.
Vilevile, Mwalimu Mkuu huyo ALIWASHUKURU  WAZAZI na Wananchi wengine waliotoa MICHANGO yao wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dr Vincent Naano, Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo na VIONGOZI wengine wa Chama (CCM) na Serikali.
Pamoja na HARAMBEE hiyo, Mwalimu Mkuu huyo aliendelea KUTAMBUA, kwa shukrani nyingi, MICHANGO ya AWALI iliyokwishatolewa Shuleni hapo kutoka kwa WADAU wengine wa Maendeleo wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, Ndugu Juma Ramadhani, Mwl Masinde Bigambo na Ndugu Paschal Rutundwe.