HATI hii ya HESHIMA ni kielelezo cha WANA-RUSOLI kutambua MCHANGO MKUBWA wa MAENDELEO anaoutoa Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwenye Kata ya Rusoli.
HATI imekabidhiwa na M/kiti wa CCM Kata ya Rusoli Ndugu Sabato Mkome, kwa Msaidizi wa Mbunge Hamisa Gamba, leo tarehe 6/9/2019, kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
ameishukuru sana CCM Kata ya Rusoli, kwa kutambua MCHANGO WAKE MKUBWA kwenye Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2015-2020) kwenye Kata hiyo na ndani ya Kata zote za Jimbo la Musoma Vijijini.