MAHAFALI YA DARASA LA VII YATUMIKA KUBORESHA MIUNDOMBIMU YA SHULE 2 ZA MSINGI

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo AKIKABIDHI Saruji Mifuko 100 na Fedha taslimu na Milango 2 (Tsh 300,000) kwenye S/M Nyaminya A & B Kijijini Tegeruka, Kata ya Tegeruka.

23 Oktoba 2019
Jimbo la Musoma Vijijini
MAHAFALI ya Darasa la VII ya tarehe 23.08.2019 ya Shule za Msingi Nyaminya A na B yametumika kuharakisha ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa na Ofisi za Walimu za Shule hizo mbili zilizoko Kijijini Tegeruka, Kata ya Tegeruka.
MGENI RASMI wa MAHAFALI hiyo alikuwa Ndugu SHAIBU NGETICHA, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mara.
MATOKEO YA MITIHANI ya Wahitimu hao ni haya hapa – haya ni kwa Watahiniwa wasiozidi 40 ndani ya Darasa (S/M Nyaminya A&B zilikuwa na Watahiniwa chini ya 40).
(i) S/M Nyaminya A
*Imeshika nafasi ya KWANZA (1) kwenye Kata yao yenye Jumla ya Shule za Msingi 6.
*Imeshika nafasi ya 3 kati ya Shule za Msingi 26 za Halmashauri ya Musoma yenye Jimbo la Musoma Vijijini
*Imeshika nafasi ya 44 kati ya Shule 158 za Mkoa wa Mara
*Imeshika nafasi ya 2,576 kati ya Shule 7,102 Taifa
Kumbuka haya MATOKEO ni kwa Watahiniwa wasiozidi 40 ndani ya Darasa.
(ii) S/M Nyaminya B
*Imeshika nafasi ya 3 kwenye Kata yao.
*Imeshika nafasi ya 14 Wilayani
*Imeshika nafasi ya 120 Mkoani Mara
“Imeshika nafasi ya 5,562 Taifa
Kumbuka haya MATOKEO ni kwa Watahiniwa wasiozidi 40 ndani ya Darasa.
Jana, tarehe 23.10.2019, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ALITIMIZA AHADI yake ILIYOTOLEWA kwenye HARAMBEE ya tarehe 23.08.2019 iliyofanyika wakati wa MAHAFALI ya Darasa la VII wa Shule hizo mbili.
Mbunge huyo ALITOA SARUJI MIFUKO 100 (kila Shule Mifuko 50) na MLANGO 2 yenye thamani ya Tsh 300,000 (kila Shule Mlango 1)