KRISMASI 2019 – WANAVIJIJI WAFURAHIA ZAWADI YA MAJENBE YA KUKOKOTWA NA NG’OMBE (PLAU)

UTOAJI wa ZAWADI YA KRISMASI ya PLAU kwa VIKUNDI 20 vya KILIMO vya Jimbo la Musoma Vijijini

VIKUNDI 20 VYA KILIMO kutoka VIJIJI 20 ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini WAMEPOKEA KWA FURAHA KUBWA Zawadi ya Krismasi kutoka kwa Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo.
ZAWADI hiyo iliyotolewa tarehe 24.12.2019 kwa kila Kikundi ni PLAU MOJA – Jembe la kukokotwa na ng’ombe moja. Mbunge huyo AMETOA ZAWADI hiyo ikiwa ni ISHARA ya kuanza rasmi KAMPENI ya kupunguza matumizi ya JEMBE la MKONO Jimboni humo.
PLAU hizo zimegawiwa kwenye Vituo 2:
KITUO 1: CHUMWI SENTA – Vikundi kutoka Vijiji vya:
Bukima, Butata, Chimati, Chitare, Chumwi, Mabui Merafuru, Masinono, Mikuyu, Kaburabura, Rusoli, Suguti na Wanyere
KITUO 2: NYASURURA SENTA – Vikundi kutoka Vijiji vya: Kamguruki, Kwibara, Maneke, Mwiringo, Nyakatende, Nyasaungu, Nyegina na Tegeruka.
MADIWANI na Viongozi wengine wa Kata zenye Vijiji vilivyopewa ZAWADI hiyo ya KRISMASI walikuwepo.
Mbunge wa Jimbo aliambatana na rafiki zake wa miaka mingi kutoka Ujerumani ambao wamemtembelea huko Jimboni. Wageni hao, Christa Werner (Dr.rer.nat.) na Wolfgang Zils (Dipl Ing, Dipl Geol) walisoma na Prof Muhongo huko Ujerumani ya Magharibi miaka ya 80.
KRISMASI YA JIMBO (2019)
Itafanyika Kijijini Nyasaungu, Kata ya Ifulifu.
HARAMBEE ya ujenzi wa Nyasaungu Secondary School, IBADA KANISANI na Chakula cha Mchana cha Krismasi (CHRISTMAS LUNCH), vyote vimefanyika Kijijini Nyasaungu,  tarehe 25.12.2019.