WANAFUNZI wa Kitongoji cha Kwisayenge, Kijiji cha Kaburabura mpakani na Wilaya jirani ya Bunda WANALAZIMIKA kutembea umbali wa kilomita usiopungua KM 15 kwenda (na kurudi umbali huo huo) MASOMONI Nyambono Sekondari ya Kata jirani ya Nyambono.
Alhamisi, 16.1.2020 SEKONDARI MPYA, DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL ya Kata ya Bugoji IMEANZA kutoa ELIMU ya SEKONDARI ndani ya Kata hiyo.
WANAFUNZI 141wa Kata ya Bugoji waliochaguliwa kuendelea na MASOMO ya Sekondari HAWATATEMBEA TENA UMBALI MREFU kwenda masomoni.
MAFANIKIO ya kuipata Dan Mapigano Memorial Secondary School yametokana na USHIRIKIANO MZURI wa SERIKALI na WANANCHI WA KATA YA BUGOJI yenye Vijiji 3 (Kaburabura, Kanderema na Bugoji)
* Wanavijiji wa Vijiji 3 wamechangia NGUVUKAZI na FEDHA.
* Viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini wamechangia FEDHA na USHAURI
* Wazaliwa wa Kata ya Bugoji. Baadhi yao walichangia FEDHA na USHAURI. Majina yataandikwa kwenye ubao na kutunzwa shuleni hapo.
*Serikali ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imechangia FEDHA, USHAURI na UONGOZI chini ya Mkuu wa Wilaya ya Musoma (Dr Vicent Naano Anney) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yetu (Ndg John Lipesi Kayumbo). PONGEZI za dhati kwa Viongozi hao na TIMU zao za kazi.
*Diwani wa Kata ya Bugoji, Mhe Ibrahimund Malima na TIMU zake za UJENZI na UONGOZI zinapewa PONGEZI nyingi za dhati kwa kazi nzuri mno. Vilevile, Mtendaji Kata, Ndugu Edna Edward Kurata na TIMU yake ya kazi wanastahili PONGEZI nyingi kwa UTEKELEZAJI mzuri wa majukumu yao.
UJENZI ULIOVUNJA REKODI
*Ujenzi wa Dan Mapigano Memorial Secondary School ulianza DISEMBA 2018 na kufikia NOVEMBA 2019 tayari MIUNDOMBINU muhimu ilishakamilishwa (k.m. Vyumba 5 vya Madarasa, Madawati, Ofisi 2 za Walimu, Vyoo matundu 10, misingi ya ujenzi wa Maabara na Nyumba ya Walimu)
HAKUNA MISANGAMANO MADARASANI
*Wanafunzi 141 wa Form I wanatumia VYUMBA 3 vya MADARASA (kwa sasa vipo 2 vya ziada). Kila Mwanafunzi analo DAWATI lake na KITI chake.
OFISI 2 ZA WALIMU
* Kwa sasa wapo WALIMU 5, yaani Headmaster na Walimu wake 4. Ofisi na samani zinatosha.
VYOO VYA WANAFUNZI & WALIMU
* Mashimo 10 ya Wasichana, 10 ya Wavulana na 2 ya Walimu yanatosha.
UJENZI WA VIWANGO BORA UNAENDELEA
* Ujenzi wa Maabara, Madarasa mengine, Maktaba, Nyumba za Walimu na Viwanja vya Michezo UNAENDELEA.
KUJIPONGEZA NA KUENDELEA NA UJENZI KWA KASI na UMAKINI MPYA
*Jumanne, tarehe 25 Februari 2020, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwa kushirikiana na WAZALIWA wa Kata ya Bugoji WALIFANYA TAFRIJA Shuleni hapo (Dan Mapigano Memorial Secondary School) ya KUWAPONGEZA WANAVIJIJI wa Kata ya Bugoji kwa hatua hiyo waliyoifikia kwenye ujenzi wa Sekondari yao ya Kata – hawakuwa nayo!