Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini lenye VITONGOJI 374, VIJIJI 68 na KATA 21 lina Jumla ya SHULE za MSINGI 111 za SERIKALI, 3 za BINAFSI na SHULE SHIKIZA 11 zinajengwa na nyingine tayari zimekamilika na kuanza kutumiwa.
TATIZO kubwa kwenye Shule za Msingi ni UKOSEFU na UPUNGUFU wa Vyumba vya MADARASA kunakosababisha MIRUNDIKANO Madarasani na kuwepo kwa MADARASA CHINI YA MITI. Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini WAMEDHAMIRIA KUTATUA TATIZO la kuwepo kwa Madarasa CHINI YA MITI.
Kijiji cha Bwasi kilichopo Kata ya Bwasi chenye VITONGOJI 5 na KAYA 450 wameanza ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa kutokana na upungufu mkubwa wa Madarasa unaozikabili S/M Bwasi (ilifunguliwa Mwaka 1952) na S/M Bwasi B (ilifunguliwa Mwaka 2015)
Mwalimu Mkuu wa S/M Bwasi B, Mwl Masillingi Maira amesema shule yake ina jumla ya Wanafunzi 508 (uandikishaji bado unaendelea), wana Vyumba 4 vya Madarasa na UPUNGUFU wa Vyumba 8 vya Madarasa. Mwalimu Mkuu huyo ameeleza kwamba Darasa lenye WANAFUNZI WENGI linao 136 kwenye Chumba kimoja na lisilokuwa na MRUNDIKANO darasani lina Wanafunzi 34. Kwa hiyo, Madarasa 4 YANASOMEA NJE, CHINI YA MITI.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Bwasi, Ndugu Mbeli Mkama Majinge ameeleza kuwa walifanya KIKAO na kuafikiana kwamba KILA KITONGOJI kijenga CHUMBA KIMOJA kwa kutumia MICHANGO YA WANAVIJIJI ya kila Kitongoji. Kwa mfano, Kitongoji cha Mtakuja kila KAYA inachangia Tsh 58,000, hatua kwa hatua, hadi ukamilishaji wa ujenzi wao.
Mtendaji Kata, Ndugu Mashaka Kagere amesema WANAVIJIJI WAMEHASIKA kujenga Vyumba vipya 5 vya Madarasa na Ofisi 3 za Walimu. Ndugu Kagera amesema VYUMBA 4 vya Madarasa VITAKAMILIKA kabla ya tarehe 29.2.2020 na MAJENGO mengine yatakamilishwa ifikapo tarehe 30.5.2020
VIONGOZI wa Kata ya Bwasi WANAMSHUKURU SANA Mkuu wa Wilaya, Dr Vicent Naano Anney kwa KUHAMASISHA Wananchi wa Kata hiyo (hasa Vijiji vya Bugunda na Bwasi) KUANZA UJENZI wa Vyumba Vipya vya Madarasa. Ujenzi ULIKUWA UMEKWAMA kwa muda mrefu.
Aidha Diwani wa Kata hiyo, Mhe Masatu Nyaonge anatoa shukrani za dhati kwa Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo kwa KUENDELEA KUHAMASISHA WANAVIJIJI kwenye masuala la MAENDELEO kwenye Kata yao likiwemo hili la UJENZI wa Vyumba Vipya vya Madarasa na KUACHANA na MADARASA CHINI YA MITI.
Katika UBORESHAJI wa ELIMU kwenye Kijiji cha Bwasi, Mbunge wa Jimbo, Profesa Muhongo aliwahi kuchangia vifuatavyo:
S/M Bwasi
*Madawati 39
*Vitabu vingi vya Maktaba
S/M Bwasi B
*Madawati 36
*Saruji Mifuko 70
*Vitabu vingi vya Maktaba
WAZALIWA WA KATA YA BWASI, WATU WALIOSOMA S/M BWASI na BWASI Sekondari WANAOMBWA KUCHANGIA UJENZI wa KUTOKOMEZA MADARASA CHINI YA MITI! KARIBU UCHANGIE.