SEKONDARI MPYA ILIYOFUNGULIWA MWAKA HUU (2020) YAJITAYARISHA KUPOKEA WANAFUNZI WAPYA MWAKANI (2021)

AWAMU YA PILI ya ujenzi wa MIUNDOMBINU ya Busambara Sekondari ya Kata ya Busambara Inaendelea vizuri.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
BUSAMBARA SEKONDARI ya Kata ya Busambara imefunguliwa Januari 2020 na inao WANAFUNZI 130 wa KIDATO cha KWANZA ambao wana VYUMBA 3 vya MADARASA na kila Mwanafunzi analo DAWATI lake na KITI chake – HAKUNA MIRUNDIKANO MADARASANI –  SHUKRANI nyingi ziende kwa Benki ya NMB kwa kuchangia Madawati na Viti hivyo.
WANANCHI wa VIJIJI 3 vya Kata ya Busambara (VIJIJI: Kwikuba, Maneke na Mwiringo), wameanza UJENZI MPYA kwa ajili ya  kupokea WANAFUNZI wa KIDATO cha KWANZA mwakani (Januari 2021)
WAZALIWA wa VIJIJI  hivyo WANAENDELEA KUCHANGIA ujenzi wa SEKONDARI ya Kata yao.
AFISA MTENDAJI wa Kata ya Busambara, Ndugu Victor Kasyupa ameeleza kuwa SEKONDARI hiyo mwakani (Januari 2021) inataraji kupokea WANAFUNZI 270 wa KIDATO cha KWANZA (2021).
Kwa hiyo, SEKONDARI hiyo ina MAHITAJI ya VYUMBA VIPYA 7 vya MADARASA. Kipo chumba kimoja,  na vinahitajika 6 vingine.
MGAWANYO WA KAZI VIJIJINI ni kama ifuatavyo:
(i) KIJIJI CHA MANEKE:
* Kumalizia Boma la Vyumba 2 vya Madarasa
(ii) KIJIJI CHA KWIKUBA:
* Kuanza ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa. Tayari wameanza kufyatua MATOFALI kwa kutumia SARUJI MIFUKO 50 iliyotolewa na Ndugu JUMA RAMADHAN, Mzaliwa wa Kijiji hicho – Tunamshukuru sana ndugu yetu huyu kwa MCHANGO wake.
(iii) KIJIJI CHA MWIRINGO:
* Kuanza ujenzi wa Vyumba 2. Tayari wameishanza kusomba mchanga.
UCHANGIAJI WA AWAMU YA KWANZA ya ujenzi wa BUSAMBARA SEKONDARI ulikuwa hivi:
(i) WANAVIJIJI
* Nguvukazi na Fedha Taslimu vyenye thamani ya Tsh 45M – HONGERENI SANA WANAVIJIJI.
(ii) FEDHA ZA SERIKALI KUU: Tsh 37.5M – SHUKRANI NYINGI KWA SERIKALI YETU.
(iii) HALMASHAURI: mbali ya kusimamia MANUNUZI ya Fedha za MFUKO wa JIMBO, Halmashauri yetu ilichangia MASINKI 14 na Fedha Taslimu Tsh 2M – Tunamshukuru sana MKURUGENZI wetu (Ndugu John Kayombo) na WAFANYAKAZI wote wa HALMASHAURI yetu.
(iv) MBUNGE WA JIMBO, Prof Sospeter Muhongo,  alichangia:
* SARUJI MIFUKO 150
* MABATI BANDO 8 (Mabati 112)
* RANGI ya kupaka Vyoo vyote
* VITABU vya Maktaba
MFUKO wa JIMBO ulichangia:
 * SARUJI MIFUKO 365
* NONDO 100
(v) WATAALAMU NGAZI YA KATA: walichangia SARUJI MIFUKO 10 – AHSANTENI SANA!
(vi) WAZALIWA 13 wa VIJIJI hivyo WALIOCHANGA kati ya Tsh 1.2M na 100,000 ni: Diwani (Chadema, amejiuzulu), Mhe Ngero Antony Kibuyu, Mwenyekiti wa Wazazi (W) Ndugu Phares Nguruti, ACP Sulemain Nyakulinga, Ndugu Joseph Chikongoye, Wakili Saidi Chiguma, Simon Songe, James Nyamanda, Alfaxad Kajanja, Obadia Nyangiro, Nyetango Kajanja, Monica Chikongoye, P Maregesi, Masondore Isarael na Michael Saire – AHSANTENI SANA!
WALIMU 2 WA KUJITOLEA: Ndugu Joseph Chikongoye,  Wakili Saidi Chiguma, Ndugu Richard Cheumbe na Thadeo Makindu WANACHANGIA POSHO za kila Mwezi za Walimu hao – AHSANTENI SANA KWA KUCHANGIA POSHO ZA WALIMU WETU!
MICHANGO YA AWAMU YA PILI YA MBUNGE WA JIMBO
MWEZI UJAO (Mei, 2020), Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ATAANZA KUCHANGIA AWAMU ya PILI ya UJENZI kwa Sekondari Mpya 2 zilizofunguliwa Januari 2020, ambazo ni: Busambara Secondary School (Kata ya Busambara) na Dan Mapigano Memorial Secondary School (Kata ya Bugoji).
OMBI KUTOKA KWA WANAVIJIJI:
TUENDELEE KUCHANGIA UJENZI WA BUSAMBARA SEKONDARI