SHULE YENYE WANAFUNZI 187 KWENYE CHUMBA KIMOJA CHA DARASA YACHANGIWA KUJENGA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA

Kazi za ujenzi zinazofanyika kwenye S/M NYAMIYENGA ya Kijijini Bwai Kumusoma, Kata ya Kiriba.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
MIUNDOMBINU ya ELIMU inaendelea KUJENGWA na KUBORESHWA kwenye SHULE ZOTE za  MSINGI (111 za Serikali, 3 za Binafsi na 11 Shule Shikizi), na SEKONDARI (20 za Serikali, 2 za Binafsi na 5 Mpya zinajengwa) ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
UJENZI na UBORESHAJI huo UNATEKELEZWA kwa USHIRIKIANO wa WANANCHI na SERIKALI yao.
SHULE YA MSINGI NYAMIYENGA
Shule hii ilifunguliwa Mwaka 2016 na iko kwenye Kijiji cha Bwai Kumusoma, Kata ya Kiriba.
S/M NYAMIYENGA ina Jumla ya WANAFUNZI 411 (Awali hadi Darasa la V) na WANAFUNZI 187 wa Darasa la III WAMERUNDIKANA kwenye Chumba kimoja cha Darasa. Walimu (jumla ni 6) hawana Ofisi na hawana Vyoo vyao.
KUTATUA MATATIZO YA S/M NYAMIYENGA
MWALIMU Heriel Joseph ambaye ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa S/M Nyamiyenga amesema kuwa HAKIPO CHUMBA CHA DARASA kwa ajili ya Darasa la VI litakalopanda kutoka Darasa la V mwakani (Januari 2021)
WANANCHI wa Kijiji cha Bwai Kumusoma   WAMEAMUA kutatua  MATATIZO hayo kabla ya kufika tarehe 30 Julai 2020.
* Kwa sasa KAMATI ya UJENZI ya Shule hiyo inasimamia UJENZI wa VYUMBA VIPYA 3 vya Madarasa, OFISI ya WALIMU na CHOO yenye MATUNDU 10.
 MICHANGO YA KUKAMILISHA UJENZI
* WANAVIJIJI wanachangia NGUVUKAZI (kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji) na FEDHA Taslimu (Tsh 5,000 kwa kila mwenye umri wa zaidi ya miaka 18) – haya yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Ndugu Sikudhani Juma Maanya.
* HALMASHAURI yetu ulishachangia Tsh Milioni 4.
* MBUNGE WA JIMBO leo (23.4.2020) amechangia SARUJI MIFUKO 50. Hapo awali alishachangia SARUJI MIFUKO 60, MADAWATI 65 na VITABU 1,000 vya MAKTABA.
OMBI KUTOKA KWA WANAVIJIJI
WADAU wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA wa KATA YA KIRIBA wanaombwa KUCHANGIA UJENZI wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye S/M NYAMIYENGA.