JIMBO la Musoma Vijijini tayari linatekeleza ILANI MPYA ya CCM (2020-2025) kwa SHULE za MSINGI kujenga MAKTABA zao.
(1) SHULE YA MSINGI RUKUBA
Hii iko Kata ya Etaro. MAKTABA imekamilika na inatumika. Ujenzi wake ni mafanikio ya USHIRIKIANO wa WANANCHI, PCI (USA – vifaa vingi vya ujenzi), PROF MUHONGO (Saruji Mifuko 50) na UONGOZI wa SHULE. VITABU vya Maktaba vilitolewa na Prof Muhongo.
VIAMBATANISHO – Picha za Jengo lenye Mabati Meupe (Maktaba) baadhi ya vitabu vimeshakabidhiwa
(2) SHULE YA MSINGI BUTATA
Hii iko Kata ya Bukima. Ujenzi wake ni mafanikio ya USHIRIKIANO wa MiCHANGO ya WANANCHI, PCI (USA – vifaa vingi vya ujenzi), PROF MUHONGO (Saruji Mifuko 50) na UONGOZI wa SHULE. VITABU vya Maktaba vitatolewa na Prof Muhongo na PCI (USA).
(3) SHULE YA MSINGI BUSAMBA
Hii iko Kata ya Etaro na inajengwa kwa USHIRIKIANO wa WANANCHI, PROF MUHONGO (Saruji Mifuko 60) na UONGOZI wa SHULE
(4) SHULE YA MSINGI BURAGA
Hii iko Kata ya Bukumi. WANANCHI wamemuomba MGOMBEA UBUNGE wa CCM (Prof Muhongo) achangie ujenzi wake baada ya Uchaguzi wa tarehe 28.10.2020. Amepokea OMBI hilo na kukubali kushirikiana na Wananchi hao.
(5) SHULE YA MSINGI BUIRA
Hii iko Kata ya Bukumi. Ujenzi wake unafanana na ule wa S/M BURAGA (soma hapo juu).
(6) AGAPE PRIMARY SCHOOL
Hii ni SHULE ya PRIVATE (Binafsi) iliyoko kwenye Kata ya Bukima na inajenga JENGO la TEHAMA (angalia Kiambatanisho – Picha za Jengo lenye mabati ya rangi ya kijani).
PROF MUHONGO alishachangia VITABU vya MAKTABA na Saruji Mifuko 50 ya ujenzi wa Jengo la Tehama la Shule hii, na alihaidi kuchangia COMPUTERS.
SHULE NYINGINE za MSINGI za JIMBO la Musoma Vijijini zimeweka MIPANGO ya ujenzi wa MAKTABA zao.
PROF MUHONGO aligawa VITABU vingi vya MAKTABA kwenye SHULE zote za MSINGI za JIMBO hili (111 za Serikali & Agape ya Binafsi).
ILANI MPYA CCM (Elimu & Mafunzo) TAYARI INATEKELEZWA ndani ya JIMBO la Musoma Vijijini
*VITENDO KWANZA
*MAENDELEO KWANZA
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
27 Sept 2020