KATA ya NYAMRANDIRIRA ina Vijiji 5 (Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka) na Sekondari moja, KASOMA SEKONDARI. Sekondari hii imeelemewa na WINGI wa WANAFUNZI wa kutoka Vijiji 5 WANAORUNDIKANA madarasani.
Baadhi ya Wanafunzi hao wanatembea UMBALI MREFU wa zaidi ya kilomita 10 kwenda masomoni kwenye Sekondari hiyo.
SULUHISHO: kujenga Sekondari ya pili ya Kata hiyo. Ujenzi umeanza na lengo kuu ni kuifungua mwakani (Januari 2021).
MAJENGO YANAYOJENGWA KWA SASA
* Vyumba 8 vya Madarasa
* Jengo la Utawala
* Vyoo vya Wanafunzi & Walimu
* Maabara
* Maktaba
* Nyumba za Walimu
MAJENGO YANAYOHITAJIKA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA MWAKANI
IDADI YA WANAFUNZI:
* Maoteo: Wanafunzi 250 wa Kata ya Nyamrandirira watafaulu kujiunga na Kidato I mwakani, Januari 2021
* Maoteo: Wanafunzi 100 watajiunga na SEKA SEKONDARI
* Wanafunzi 150 watajiunga na KASOMA SEKONDARI
MAJENGO YANAYOPASWA KUKAMILISHWA KABLA YA TAREHE 30 DISEMBA 2020:
(1) Vyumba 3 vya Madarasa
(2) Ofisi 1 ya Walimu
(3) Choo chenye Matundu 8
WANAOCHANGIA UJENZI HUU (hadi leo hii):
(1) Wanavijiji wa Vijiji 5
(2) Viongozi wa Vijiji/Kata
(3) Mgodi Mdogo wa Dhahabu wa Seka
(4) Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo (alishachangia Saruji Mifuko 150)
MABATI 54:
Tarehe 24.11.2020, Mbunge wa Jimbo, Prof S Muhongo atachangia MABATI 54 ya kuezeka Chumba 1 cha Darasa.
WAZALIWA WA KATA YA NYAMRANDIRIRA:
* Wanavijiji bado wanasubiri kwa shauku kubwa AHADI za MICHANGO ya WAZALIWA (na marafiki zao) wa Kata hiyo.
MICHANGO IPELEKWE kwa:
* Mtendaji: 0756 680 887
* DC wa Wilaya ya Musoma
* Mkurugenzi wa Halmashauri (Musoma DC)
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz