SHULE ZA MSINGI ZA MUSOMA VIJIJINI ZAENDELEA KUJENGA NA KUTUMIA MAKTABA

WANAFUNZI wakijipatia vitabu ndani ya MAKTABA yao.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Jumamosi, 21.11.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
SHULE YA MSINGI BUTATA, iliyoko Kijijini Butata, Kata ya Bukima imejenga MAKTABA MPYA kwa muda wa MIEZI 8 na tayari inatumika.
MWALIMU MKUU,  Mwl Nancy Lema amesema Shule hiyo iliyoanza Mwaka 1942, ina furaha nyingi sana ya KUPATA MAKTABA ambayo inatumiwa na WANAFUNZI wa Madarasa yote kujisomea na hasa kufanya kazi za ziada walizopewa na Walimu wao (homeworks)
MICHANGO YA UJENZI WA MAKTABA
Mwalimu Yohana Dawi, Mwalimu wa MIUNDOMBINU, aliyesimamia ujenzi wa Maktaba hii amesema MICHAGO ilitoka kwa:
*WAKIJIJI wa Kijiji cha Butata walichangia NGUVUKAZI – kusomba mawe, mchanga na maji.
* PCI (Tanzania) inapewa shukrani nyingi sana kwa kutoa Vifaa vingi vya ujenzi wa Maktaba  hii. MEZA, VITI na SHUBAKA vimetolewa na PCI (Tanzania)
* MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alichangia Shule hii  SARUJI MIFUKO 100 (50 Maktaba & 50 Vyumba vipya vya Madarasa)
* WAZALIWA 2 wa Kijiji cha Butata, Ndugu Samson Masawa (Tsh 500,000) na Masawa Masawa (Tsh 500,000) walichangia
VITABU VYA MAKTABA
Mwl Yohana Dawi amesema VITABU vya MAKTABA hiyo vimetolewa na:
* PCI (Tanzania)
* MBUNGE wa Jimbo , Prof Sospeter Muhongo
WATUMIAJI WENGINE WA MAKTABA HII
Mbali ya WANAFUNZI wa S/M Butata, WANAFUNZI wa SHULE za MSINGI na SEKONDARI jirani, na WANANCHI wa Kata ya Bukima na wengine wote WANAKARIBISHWA kutumia MAKTABA ya S/M BUTATA – Karibuni Mjisomee!
JIMBO LA Musoma Vijijini lenye Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374 lina jumla ya SHULE za MSINGI 111 (za Serikali), 3 (za Binafsi) na linajenga Shule Mpya 14 za Msingi.
*ELIMU NI INJINI YA MAENDELEO*
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini