EQUITY BANK YAINGIA MUSOMA VIJIJINI: WAVUVI WAJIUNGA  KWENYE VIKUNDI KUOMBA MIKOPO

UHAMASISHAJI wa uundwaji wa VIKUNDI vya UVUVI ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Tarehe, 16.12.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
WAVUVI walioko katika Mialo minne ya Busekera (Kata ya Bukumi), Bwai Kumusoma (Kata ya Kiriba) na Visiwa vya Iriga na Rukuba (Kata ya Etaro) wamepokea ELIMU ya kujiunga kwenye VIKUNDI vya UVUVI ili kutekeleza shughuli zao za UVUVI kwa UFANISI mkubwa zaidi, na uwezekano wa kupata MITAJI kupitia MIKOPO mbalimbali.
VIONGOZI wa HALMASHAURI ya WILAYA ya MUSOMA  waliwatembelea WAVUVI wa Kata hizo 3 na kufanya uhamasishwaji huo  kwa muda wa siku mbili mfululizo.
AFISA UVUVI wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu Augustine Constatine alisisita suala la UVUVI BORA unaozingatia SHERIA na KANUNI zake.
AFISA MAENDELEO ya JAMII wa Halmashauri hiyo, Ndugu Tanna Nyabange na Msaidizi wake Ndugu Nyanjara Majura walielezea umuhimu wa uundwaji wa VIKUNDI vya UVUVI kwa ajili ya kupata na MIKOPO kutoka kwenye HALMASHAURI yao na kutoka kwenye TAASISI za FEDHA, zikiwemo BENKI mbalimbali. Suala la upatikanaji wa SOKO ya UHAKIKA kupitia Vikundi vya Uvuvi lilisisitizwa.
WASAIDIZI 3 wa MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Ndugu Fedson Masawa, Ndugu Verediana Mgoma na Ndugu Hamisa Gamba WALISHIRIAKANA na VIONGOZI wa Halmashauri hiyo kuorodhesha VIKUNDI vya UVUVI vyenye nia ya kuomba MIKOPO  kutoka Equity Bank.
EQUITY BANK NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
BANK hiyo imewakilishwa na Ndugu Bahati Dollo, Kemilembe Kabugumila na Peter Chuchu, kwenye ZIARA ya KIKAZI ya siku 2 na kuongea na VIKUNDI vya UVUVI vya Kata hizo tatu.
IDADI ya VIKUNDI
vilivyojitokeza kuomba MIKOPO kutoka Bank hiyo ni kama ifuatavyo:
(i) Kata Bukumi (Vijiji 4)
*Vikundi 17, Wanachama 203
(ii) Kata ya Kiriba (Vijiji 3)
*Vikundi 25, Wanachama 327
(iii) Kata ya Etaro (Vijiji 3)
*Kisiwa cha Rukuba
Vikundi 31, Wanachama 425
*Kisiwa cha Iriga
Vikundi 6, Wanachama 80
EQUITY BANK itaanza na VIKUNDI vya UVUVI 79, vyenye WANACHAMA 1,035
LEO, Jumatano, 16.12.2020, MAAFISA 3 wa EQUITY BANK wameonana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney, na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo KUJADILI FURSA hiyo ya upatikanaji wa MIKOPO ya EQUITY BANK kwa VIKUNDI vya UVUVI vya Jimbo la Musoma Vijijini.
EQUITY BANK iko tayari kutoa MIKOPO kwa VIKUNDI vya UVUVI vya Jimbo la Musoma Vijijini – matayarisho yanaendelea.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini