MUSOMA VIJIJINI – RUWASA YAONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA USAMBAZAJI MAJI YA ZIWA VIKTORIA

Jumamosi, 30.1.2021 RUWASA (W) ilifanya majaribio ya MRADI wa MAJI wa BULINGA-BUJAGA kwenye KITUO cha SWEDI

INJINIA Saidi Nyamlinga, Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Musoma amesema kwamba kwenye Mradi huu wamejenga MATENKI 2:

(i) Tenki la Kijijini BULINGA lina uwezo wa kujaza LITA 150,000. VITUO 14 vimejengwa na leo (30.1.2021) majaribio yamefanywa kwenye KITUO cha Swedi – PICHA 3 za hapa zinaonesha WANAVIJIJI wakiteka MAJI kutoka Kituo cha Swedi.

Hili ni BOMBA la MAJI la Bujaga-Bulinga ndani ya Kata ya Bulinga

(ii) Tenki la Kijijini BUSUNGU lina uwezo wa kujaza LITA 225,000. Ujenzi wa VITUO 15 vya Vijiji 3 vya Busungu, Bukima na Kwikerege unakamilishwa na majaribio yatafanywa ndani ya wiki 2 zijazo.

Hili ni BOMBA la MAJI la Busungu-Bukima-Kwikerege ndani ya Kata za Bulinga, Bukima na Rusoli.

MAJARIBIO yakikamilika, WANAVIJIJI watakaribishwa kutuma MAOMBI ya kufungiwa maji majumbani mwao au kwenye maeneo ya biashara zao.

HONGERENI SANA RUWASA

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz