Tarehe 2.2.2021
Jimbo la Musoma Vijijini
HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) yenye Jimbo la Musoma Vijijini (Kata 21, Vijiji 68) lina:
*Magari ya Wagonjwa (Ambulances) 5
*Zahanati 24 za Serikali zinazotoa huduma za Afya
*Zahanati 4 za Binafsi zinazotoa huduma za Afya
*Zahanati mpya 14 zinajengwa
*Vituo vya Afya 3 vinatoa huduma za Afya
*Hospitali ya Wilaya 1 – ujenzi unakamilishwa
WANAVIJIJI wa Jimbo la Musoma Vijijini wameamua kuboresha HUDUMA za AFYA zitolewazo kwenye ZAHANATI zao kwa kujenga WODI za Mama & Mtoto.
UJENZI wa MIUNDOMBINU hii mipya unachangiwa na:
*Serikali
*Wanavijiji
*Mbunge wa Jimbo
*Madiwani
*Wazaliwa wa Musoma Vijijini
*Wadau wengine wa Maendeleo
UJENZI WA WODI ZA MAMA & MTOTO
Baadhi ya ZAHANATI zilizojengwa zamani zimeanza kuboresha HUDUMA za AFYA wanazozitoa kwa kujenga WODI za Mama & Mtoto.
KISIWA cha RUKUBA ni Kijiji cha Kata ya Etaro. Kijiji hiki kimeamua kujenga WODI ya Mama & Mtoto inayotarajiwa kukamilika kabla ya tarehe 1 Machi 2021.
Zahanati nyingine zilizoanza ujenzi wa Wodi za Mama & Mtoto ni Zahanati za Bukima na Nyegina.
JENGO la WODI ya Mama & Mtoto la Zahanati ya Kisiwani Rukuba lina VYUMBA 13. Michango ya ujenzi imetolewa na:
*WANAVIJIJI – nguvukazi
*FEDHA zinazorudishwa (20% ya Makusanyo ya ushuru) kutoka Halmashauri yetu
*MBUNGE wa JIMBO – ameanza kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 200.
WADAU wa MAENDELEO wanaombwa kuanza kuchangia VIFAA vinavyohitajika kwenye WODI hiyo, vikiwemo, vitanda, magodoro, n.k.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz