Tarehe 7.4.2021
Musoma Vijijini
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SERIKALI yetu imetoa SHILINGI 31,936,072.11 (Tsh Milioni 31.94) kuchangia ujenzi wa VYOO VIPYA kwenye Shule ya Msingi LYASEMBE ya Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi.
WANAKIJIJI wamejitolea kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji (NGUVUKAZI) kwa ajili ya ujenzi wa MATUNDU MAPYA 22 ya CHOO KIPYA cha Shule yao ya Msingi.
MWALIMU MKUU wa Shule hiyo, Mwl Athuman Mnkende amesema Shule ilianza Mwaka 1975 na ina jumla ya WANAFUNZI 872.
SHULE hiyo inapaswa kuwa na MATUNDU 40 ya CHOO. Ujenzi wa kutumia FEDHA zilizotolewa na SERIKALI, na NGUVUKAZI za WANAKIJIJI, umewezesha kukamilisha CHOO KIPYA chenye MATUNDU 22 na kufanya Shule hiyo kuwa na VYOO 2 vyenye jumla ya MATUNDU 28 (13 Wasichana, 13 Wavulana na 2 Walimu).
MWALIMU MKUU huyo anaishukuru sana SERIKALI yetu kwani vyoo vilivyokuwa vinatumiwa ni vya muda mrefu (1975) na vilikaribia kujaa. Kwa hiyo, bila msaada wa SERIKALI, Shule ingalifungwa kwa kukosa Vyoo vya Wanafunzi.
MTENDAJI wa Kijiji cha Lyasembe, Ndugu Chikonya Chikonya anawashukuru sana WANAKIJIJI kwa MCHANGO wa NGUVUKAZI zao uliowezesha ujenzi kukamilika ndani ya muda uliopangwa.
DIWANI wa Kata ya Murangi, Mhe Hamisi Nyamamu amewasihi wanafunzi na walimu kutunza na kudumisha usafi wa choo hicho kipya ambacho kimejengwa kwa USHIRIKIANO wa Serikali yetu na Wananchi wa Kijiji cha Lyasembe.
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameishaichangia S/M Lyasembe:
*Madawati 80
*Vitabu vingi vya Maktaba
TUCHANGIE UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA S/M LYASEMBE
*Madarasa yanayohitajika ni 20 yaliyopo ni 10
MATOKEO YA MITIHANI YA MWAKA JANA (2020)
*STD IV (2020)
Watahiniwa 104
Waliofaulu 99 (95.2%)
*STD VII (2020)
Watahiniwa 70
Waliofaulu 43 (61.4%)
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz