VIKUNDI VYA KILIMO VYAENDELEA KUNEEMEKA KWA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NA KWA KUTUMIA PLAU 

WANACHAMA wa Kikundi cha JIPE MOYO cha Kijijini Kome, Kata ya Bwasi, wakitayarisha SHAMBA lao la MIHOGO.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
KIKUNDI cha KILIMO  cha JIPE MOYO cha Kijijini Kome, Kata ya Bwasi kinajishughulisha na KILIMO cha UMWAGILIAJI.
KATIBU wa Kikundi hiki, Ndugu Deborah Isaack, amesema kuwa KIKUNDI chao kina WANACHAMA 35 na kilianzishwa Mwaka 2015.
KIKUNDI hiki (JIPE MOYO) kinaundwa na WANAWAKE tu na wanajishughulisha na KILIMO kwa MPANGILIO ufuatao:
MAZAO YA UMWAGILIAJI (bustani): Wanalima matikiti, nyanya, vitunguu na kabeji
MAZAO YA KUTEGEMEA MVUA: Wanalima mahindi, mihogo, maharage na alizeti (majaribio)
ZANA & MBEGU ZA KILIMO
Kikundi cha JIPE MOYO kimepewa misaada na mikopo kutoka kwa : HALMASHAURI yetu (Musoma DC) imetoa MIKOPO kwa awamu mbili, yaani, MILIONI tano (5) na MILIONI saba (7).
PCI (TANZANIA) imechangia: *MASHINE ya UMWAGILIAJI, *MBEGU za mahindi na mihogo
MBUNGE wa Jimbo lao, Prof Sospeter Muhongo amechangia:
*Jembe la kukokotwa na ng’ombe (PLAU)
*MBEGU za mihogo, mtama na alizeti.
MAFANIKIO YA KIKUNDI CHA JIPE MOYO
MWANACHAMA, Ndugu Bilenjo Mangano, amesema tayari yeye AMEJENGA NYUMBA BORA na anasomesha vizuri WATOTO wake kutokana na  MAPATO mazuri ya Kikundi chao.
VIlevile, MWANACHAMA huyo amesema wenzake wengine wamefanikiwa kufungua MADUKA kutokana na MAPATO mazuri ya Kikundi chao.
SHULE YA MSINGI KOME YAPEWA CHAKULA
Kikundi cha JIPE MOYO kimegawa sehemu ya MAVUNO yake ya hivi karibuni na kuipatia S/M Kome:
*MAHINDI Magunia 4
*MAHARAGE kilo 80
AFISA KILIMO wa  Kata ya Bwasi, Ndugu Alex Mihambo, amekuwa akifuatilia kazi za KILIMO za Kikundi hikil na kuhakikisha kuwa SOKO la MAZAO yao linapatikana bila usumbufu.
AFISA Kilimo huyo  amesema kwamba WANAVIJIJI wengine wamehamasika sana na KUANZISHA VIKUNDI vya KILIMO na kwa sasa kuna VIKUNDI vipya 15 Kijijini Kome.
KIKUNDI CHA JIPE MOYO CHATAYARISHA MIRADI MIPYA
Kwa siku za usoni, Kikundi hiki kimepanga kufanya yafuatayo:
*Kuongeza HISA za MFUKO wao wa FEDHA za kukopeshana
*Uoteshaji wa MITI ya msitu
*Ufugaji wa NYUKI kwa ajili ya biashara ya ASALI
*Kuanzisha KIWANDA kidogo cha kukamua MAFUTA ya ALIZETI.
DC, DED, MBUNGE, MADIWANI na VONGOZI wengine wanawashawishi WANAVIJIJI wa Jimbo la Musoma Vijijini KUANZISHA VIKUNDI VYA UCHUMI, yaani, vya Kilimo cha Umwagiliaji, Uvuvi wa samaki, Ufugaji wa nyuki, n.k.
MWITIKIO wa uanzishwaji wa VIKUNDI vya UCHUMI ni mzuri na Mbunge wa Jimbo anaendelea kugawa bure MAJEMBE ya kukokotwa na ng’ombe (PLAU) kwenye VIKUNDI vya KILIMO.
Taratibu za VIKUNDI vya UVUVI kupewa MIKOPO ya RIBA NAFUU unaendelea.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini