Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
SHULE ya MSINGI ETARO ilifunguliwa Mwaka 1995. Shule hii iko Kijijini Etaro, Kata ya Etaro.
MWALIMU MKUU wa Shule hii, Mwl Mangire Mahombwe ameeleza yafuatayo:
*Shule ina jumla ya Wanafunzi 1,079 na ina Walimu 14.
*Shule ina Vyumba vya Madarasa 9, vinavyohitajika ni 23.
*Mirundikano madarasani ni mikubwa mno. Kwa mfano, Darasa la Saba (VII), Wanafunzi wote 154 wanasomea kwenye chumba kimoja (1) cha darasa.
*Shule ina matundu 30 ya choo, yanayohitajika ni 48.
UONGEZAJI WA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA NA OFISI YA WALIMU
UJENZI wa Vyumba vipya vitano (5) vya Madarasa na Ofisi moja (1) ya Walimu wa Shule hii ulianza Mwaka 2017.
MICHANGO YA UJENZI WA VYUMBA VIPYA 5 VYA MADARASA & OFISI 1 YA WALIMU
MTENDAJI wa KIJIJI cha Etaro (VEO), Ndugu Sophia Anthony ameelezea uchangiaji wa ujenzi unaondelea kwenye S/M ETARO ni kama ifuatavyo:
*NGUVUKAZI za Wanakijiji cha Etaro: wanasomba mawe, kokoto, mchanga na maji
*FEDHA taslimu, Tsh 10,000/= (elfu kumi) zinachangwa kutoka kila KAYA. Kijiji kina KAYA 556.
*PCI Tanzania imejenga matundu 10 ya choo – Ahsante sana PCI Tanzania!
*MNARA wa SIMU, HALOTEL umechangia
(i) Saruji Mifuko 60
(ii) Mabati 54
(Ahsante sana HALOTEL)
*MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo, amechangia:
(i) Saruji Mifuko 60
(ii) Mabati 54
(iii) Madawati 227
(iv) Vitabu vya Maktaba zaidi ya 1, 000 (elfu moja)
*MFUKO wa JIMBO umechangia:
(i) Mabati 244
*MKUU wa MKOA, Marehemu Mhe Tupa: Mwaka 2012, alitoa Tsh. MILIONI 10 kwa ajili ya Mradi wa Maji Kata ya Etaro.
Kata hiyo ilipopata Mradi mwingine wa Maji, fedha hizo zimetumika kwenye ujenzi huu.
UFAULU WA S/M ETARO
Mbali ya upungufu mkubwa wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye Shule hii, UFAULU wake ni wa kuridhisha:
MATOKEO YA DARASA LA IV (2020):
* Watahiniwa 96
* Waliofaulu 93
MATOKEO YA DARASA LA VII (2020):
* Watahiniwa 90
* Waliofaulu 72
OMBI KUTOKA KWA WANAKIJIJI CHA ETARO
WAZALIWA wa Kijiji cha Etaro na Kata ya Etaro kwa ujumla, na WADAU wengine wa MAENDELEO, wanaombwa KUCHANGIA ujenzi na uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye Shule yao (S/M Etaro).
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Attachments area