Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
UONGOZI wa Serikali ya Kijiji cha Nyambono kwa kushirikiana na Wananchi wa Kijiji hicho wameanza kutekeleza MRADI wa ujenzi wa VYUMBA VIPYA 17 vya Madarasa kwenye Shule yao ya Msingi, S/M NYETASYO.
Shule ya Msingi Nyetasyo ni moja kati ya Shule mbili za Msingi zilizopo Kijijini Nyambono.
Shule hii ilianzishwa Mwaka 1944 ikiwa inamilikiwa na Kanisa la Mennonite. Mwaka 1978, Shule ilitaifishwa na Serikali.
MWALIMU MKUU wa S/M Nyetasyo, Mwl Rutoryo Hitra ameelezea MAHITAJI ya Shule hiyo kama ifuatavyo:
*Jumla ya Wanafunzi ni 873
*Vyumba vya Madarasa vinavyohitajika ni 23, vilivyopo ni 6
*Madarasa yanayosomea nje ni mawili (Darasa la Awali na Darasa la II).
MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani ni mikubwa:
*Darasa la III lina chumba kimoja chenye Wanafunzi 121
*WALIMU wanaohitajika ni 23, waliopo ni 9
*NYUMBA za Walimu zinahitajika 23, zilizopo ni 4
*VYOO vya Wanafunzi – yanahitajika Matundu 39, yaliyopo ni 10
*CHOO cha Walimu – yanahitajika Matundu 2, hakuna hata tundu moja.
UFAULU wa MITIHANI kwenye S/M NYETASYO:
*DARASA la IV (2020)
Watahiniwa: 113
Waliofaulu: 110
*DARASA la VII (2020)
*Watahiniwa: 62 *Waliofaulu: 45
WANAKIJIJI WAFANYA MAAMUZI YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SHULE YAO
AFISA MTENDAJI (VEO) wa Kijiji cha Nyambono, Ndugu Mugeta Kaitira amesema SERIKALI ya KIJIJI chao imekubaliana na WANAKIJIJI kuanza kutekeleza MRADI wa ujenzi wa Vyumba vipya 17 vya Madarasa ya Shule yao, na kwamba WANAKIJIJI watachangia:
*FEDHA taslimu, Tsh 11,500/= kutoka kila kaya
*NGUVUKAZI ya kusomba mchanga, mawe, kokoto na maji ya ujenzi.
MICHANGO ILIYOKWISHATOLEA
*MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo ameishatoa michango yake kama ifuatavyo:
(i) Madawati 60
(ii) Vitabu zaidi ya 1,000 vya Maktaba
*MFUKO wa JIMBO
(i) Tsh Milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vipya vitatu (3) vya Madarasa.
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA NYAMBONO
Wananchi wa Kijiji cha Nyambono wanawaomba WAZALIWA wa Kijiji hicho, na WADAU mbalimbali wa MAENDELEO wawaunge kwenye MIRADI ya ujenzi na uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye S/M NYETASYO
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini