Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SHULE ya MSINGI KOME B ilifunguliwa Mwaka 2015, Kijijini Kome, Kata ya Bwasi.
KATA ya BWASI ina Vijiji 3 (Bugunda, Bwasi na Kome) na kila Kijiji kina Shule za Msingi mbili (yaani shule moja kila kijiji yenye A&B).
MWALIMU MKUU wa S/M BWASI B, Mwl Yoel Peter ametoa maelezo ya Shule hiyo kama ifuatavyo:
*Jumla ya Wanafunzi ni 565
*Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 10, vilivyopo ni 6
*Mirundikano ya Wanafunzi madarasani ni mikubwa, kwa mfano Darasa la III lenye Wanafunzi 160 wana chumba kimoja cha darasa.
*Wapo Wanafunzi wenye madarasa chini ya MITI.
MICHANGO YA UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE S/M KOME B
MTENDAJI wa KIJIJI (VEO) cha Kome, Ndugu Fredrick Jeremia amesema WANAKIJIJI WAMEAMUA kuanza ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa na Ofisi ya Walimu kwenye Shule yao (S/M Kome B).
WANAKIJIJI wanachangia:
*NGUVUKAZI zao kwa kuchimba misingi ya majengo, na kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi.
*FEDHA taslimu Tsh 2,300/= kutoka kila kaya.
*SERIKALI, kupitia Mradi wake wa PEDP (Primary Education Development Programme) imetoa Tsh MILIONI 12.5 kwa ajili ya kukamilisha Chumba 1 cha Darasa na kununua madawati na meza.
MICHANGO MINGINE ILIYOKWISHA KUTOLEWA SHULENI HAPO
*SERIKALI kupitia Mradi wake wa EP4R ilitoa Tsh MILIONI 5
*PCI Tanzania imejenga Choo chenye Matundu 10
*MBUNGE wa JIMBO, Profesa Sospeter Muhongo ameishachangia:
(i) Madawati 62
(ii) Saruji Mifuko 120
(iii) Vitabu zaidi ya 1,000 vya Maktaba
*MFUKO wa JIMBO ulinunua Mabati 126
UFAULU WA MITIHANI KWENYE S/M KOME B
*Darasa la IV (2020)
Watahiniwa 36
Waliofaulu 36
*Darasa la VII (2020)
Watahiniwa 33
Waliofaulu 30
WAZALIWA wa Kijiji cha Kome na Kata ya Bwasi WANAOMBWA wachangie MAENDELEO ya nyumbani kwao – OMBI kutoka kwa ndugu zao.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini