Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
KIJIJI cha BUGUNDA kilichoko Kata ya Bwasi kina SHULE MBILI za MSINGI – S/M Bulinga na S/M Bulinga B
MWALIMU MKUU wa S/M Bulinga, Mwl Alexander Materu ameeleza yafuatayo kuhusu Shule hiyo:
*Ilifunguliwa Mwaka 1942 na kwa sasa ina jumla ya Wanafunzi 662
*Idadi ya Walimu wanaohitajika ni 15, waliopo ni 7
*Vyumba vya Madarasa vinavyohitajika ni 14, vilivyopo ni 6
*Mirundikano ya Wanafunzi madarasani ni mikubwa sana, kwa mfano, Wanafunzi 147 wa Darasa la III wanatumia chumba kimoja cha darasa.
*Jumla ya WANAFUNZI 214 wanasomea nje, chini ya miti.
MCHANGO WA SERIKALI WA KUTATUA TATIZO LA UKOSEFU WA VYUMBA VYA MADARASA
*SERIKALI kupitia Mradi wake wa EP4R imetoa SHILINGI MILIONI 40 kwa ajili ya kukamilisha Vyumba vipya viwili vya Madarasa, Ofisi 1 ya Walimu na ununuzi wa Madawati.
MICHANGO YA WANAKIJIJI KWENYE UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA YA SHULE YAO
*MTENDAJI KATA, Ndugu Mashaka Kagere amesema WANAKIJIJI wanashiriki katika ujenzi huo kwa kufanya yafuatayo:
(i) kuchimba Msingi wa Vyumba vipya 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu
(ii) kusomba mawe, mchanga na maji ya ujenzi
MICHANGO MINGINE ILIYOKWISHATOLEWA KWENYE S/M BULINGA
*PCI Tanzania ilijenga Matundu 8 ya Choo cha Wanafunzi
*MBUNGE wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo ameshachangia:
(i) Madawati 46
(ii) Vitabu zaidi ya 1,000 vya Maktaba
*MFUKO wa JIMBO
(iii) Mabati 54
*Halmashauri yetu ilishachangia Shilingi Milioni 5.
UFAULU WA MITIHANI WA S/M BULINGA
*MATOKEO Darasa la IV (2020)
Watahiniwa 85
Waliofaulu 85
*MATOKEO Darasa la VII (2020)
Watahiniwa 32
Waliofaulu 31
SHUKRANI KUTOKA KIJIJI CHA BUGUNDA
*Wanakijiji na Viongozi wao wanaishukuru sana SERIKALI kwa MCHANGO wake wa SHILINGI MILIONI 40.
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA BUGUNDA
*WAZALIWA wa Kijiji cha Bugunda na Kata ya Bwasi kwa ujumla wake, na WADAU wengine wa MAENDELEO wanaombwa wachangie ujenzi wa MIUNDOMBINU ya ELIMU ya SHULE KONGWE (S/M Bulinga) iliyofunguliwa Mwaka 1942.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini