FEDHA ZA COVID-19 KUPELEKA MAJI YA BOMBA KWENYE VIJIJI VITATU (3)

Tenki la Maji (Lita 200,000 – lenye ngazi pichani) ya Vijiji vya Saragana, Nyambono na Mikuyu lililojengwa Mlimani Nyaberango, Kijijini Nyambono

JIMBO la Musoma Vijijini limepata Tsh MILIONI 500 za COVID-19 kwa ajili ya kusambaza maji vijijini mwetu.
MATUMIZI YA FEDHA hizo za COVID-19 ni kama ifuatavyo:
*Ujenzi wa TENKI la MAJI la mita za ujazo 200 (lita 200,000) Mlimani Nyaberango, Kijijini Nyambono.
*Usambazaji wa MABOMBA ya Maji kutoka kwenye TENKI hilo kwenda Vijiji vya KANDEREMA, BUGOJI na KABURABURA.
*Mlimani Nyaberango (Kijijini Nyambono) tayari lipo TENKI la MAJI (200 cu.m./lita 200,000) kwa ajili ya MAJI ya Vijiji vya SARAGANA, NYAMBONO na MIKUYU. Tenki hili limejengwa kwa kutumia Fedha za Bajeti za Mwaka 2019/2020
CHANZO CHA MAJI YA BOMBA YA VIJIJI HIVI SITA (6)
*Fedha za Bajeti ya Mwaka 2019/2020 na Mwaka 2020/2021 zimewezesha ujenzi wa MIUNDOMBINU ya kutumia Maji ya Ziwa Victoria kutoka kwenye chanzo kilichopo Kijijini Suguti.
*Maji ya kutoka Kijijini SUGUTI yanapelekwa hadi Kijijini CHIRORWE ambapo mabomba yametandazwa kupeleka maji Kijijini WANYERE na mengine kupeleka maji, kupitia Mlima Nyaberango, kwenda Vijijini SARAGANA, NYAMBONO na MIKIYU.
OMBI KWA WANAVIJIJI
*Wanavijiji wa vijiji vyote 6 wanaombwa kurahisisha upatikanaji wa maeneo ya kutandaza mabomba ya kusafirisha maji yatakayo kuwa kwenye MATENKI 2 Mlimani Nyaberango.
*Wanavijiji wanaombwa kuchangia NGUVUKAZI kuchimba mitaro ya kutandaza mabomba ya maji – tujitolee na tuchangie upatikanaji wa MAJI ya BOMBA Vijijini mwetu.
KUKAMILIKA KWA MRADI HUU
*Imepangwa kwamba, ifikapo tarehe 30 Disemba 2021, MAJI ya BOMBA yaanze kutumika ndani ya VIJIJI 6 vya: MIKUYU, NYAMBONO, SARAGANA, KANDEREMA, BUGOJI na KABURABURA.
SHUKRANI:
*Shukrani za dhati zinatolewa na Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini kwenda kwa SERIKALI YETU, na haswa kwa MHE RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MHE SAMIA SULUHU HASSAN, kwa kufanikisha upatikanaji wa FEDHA za COVID-19 na nyingine kwa manufaa ya TAIFA LETU.
Taarifa kutoka:
*Ofisi ya RUWASA
Musoma DC
*Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini