KIJIJI CHA PEMBEZONI CHA WAFUGAJI CHA NYASAUNGU KIMEAMUA KUJENGA SEKONDARI YAKE

Wana-Nyasaungu wanapenda WATOTO wao 70 wa Kidato cha kwanza (2022) waanze masomo kwenye Sekondari yao waliyoanza kuijenga tokea Juni 2019.

Kijiji cha NYASAUNGU ni moja ya Vijiji 3 (Kabega, Kiemba & Nyasaungu) vya Kata ya IFULIFU. Hii ndiyo Kata pekee ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini ambayo haina Sekondari yake – ujenzi wa Sekondari 2 ulishaanza vijijini Kabegi (Ifulifu Sekondari) na Nyasaungu (Nyasaungu Sekondari)
Kijiji cha Nyasaungu kiko pembezoni na umbali kutoka vijiji vingine viwili vya Kata hiyo haupunguwi kilomita 10.  Wakazi wake wengi ni WAFUGAJI.
WANAFUNZI wa Sekondari wa kutoka Kijiji hiki wanaenda kusoma Sekondari za Kata za jirani ambazo ni Mugango na Nyakatende.
UMBALI wa kwenda na kurudi kwenye Sekondari hizo za Kata jirani ni takribani KILOMITA 20.
SERIKALI imetoa Tsh Milioni 470 kujenga Sekondari ya Kata ya IFULIFU ambayo itajengwa kwenye Kijiji cha KABEGI  ambacho kiko takribani KILOMITA 10 kutoka Kijijini NYASAUNGU.
Kwa hiyo, Kijiji cha NYASAUNGU kinaendelea na ujenzi wa Sekondari yake ili kutatua TATIZO la UMBALI (na madhara yake) linalowakabili watoto wao.
UJENZI wa Sekondari ya Kijiji hicho ulianza JUNI 2019 na MICHANGO ya UJENZI inatoka kwa:
*Wanakijiji:
Wanachangia nguvukazi na fedha taslimu (Tsh Milioni 19.7) kwa kuuza mifugo yao. Wasikilize kwenye CLIP iliyowekwa hapa.
*Mbunge wa Jimbo:
ameishachangia Mabati 108, Saruji Mifuko 30 na Nondo 20
*Mfuko wa Jimbo:
umeishachangia Mabati 54 na Saruji Mifuko 80
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA NYASAUNGU
*Wana-Nyasaungu wanapenda WATOTO wao 70 wa Kidato cha kwanza (2022) waanze masomo kwenye Sekondari yao waliyoanza kuijenga tokea Juni 2019.
NB: Kijiji cha Nyasaungu –  kimesimamisha ujenzi wa Zahanati ya Kijiji chao ili wakamilishe ujenzi wa Sekondari hiyo.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini