TAIFA LINAHITAJI WANASAYANSI WENGI NA MAHIRI – MUSOMA VIJIJINI KUANZA KUWA NA HIGH SCHOOLS ZA SAYANSI

Musoma Vijijini

Tumepanga tuwe na High Schools angalau 5 za masomo ya sayansi ifikapo 2025.

Jimbo la Musoma Vijijini linayo HIGH SCHOOL moja tu, nayo ni ya masomo ya ARTS (HKL, HGK na HGL). Hii ni Kasoma High School iliyoanza Mwaka 2014, na ni sehemu ya Sekondari ya Kasoma iliyofunguliwa Mwaka 1995.

Jimbo letu lina jumla ya:

*Sekondari 22 za Kata/Serikali
*Sekondari 2 za Binafsi (Madhehebu: Sabato & Katoliki)

Wananchi ndani ya Kata 21 za Jimbo letu wamepanga na wengine wameanza ujenzi wa Sekondari Mpya 10 – moja (Ifulifu Sekondari) ikiwa imepokea kutoka Serikalini Tsh MILIONI 470 za ujenzi wa Sekondari ya Kata hiyo itakayofunguliwa Juni 2022.

UJENZI NA UBORESHAJI WA MAABARA

WANAVIJIJI, kwa kushirikiana na SERIKALI yetu, wameamua kujenga na kuboresha MAABARA zote za Sekondari zetu. MAABARA hizo ni za masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia.

Mbali ya kuboresha uelewa na ufundishaji wa masomo hayo kwa WANAFUNZI wa KIDATO cha I hadi IV, lengo jingine ni kuanzisha HIGH SCHOOLS za MASOMO ya SAYANSI (k.m., PCM & PCB) Jimboni mwetu.

Tumepanga tuwe na High Schools angalau 5 za masomo ya sayansi ifikapo 2025.

WANAVIJIJi wa Kata ya Kiriba yenye Vijiji 3 wameamua kujenga MIUNDOMBINU ya HIGH SCHOOL ya masomo ya SAYANSI – tafadhali wasikilize kwenye CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.

SHUKRANI zinatolewa kwa:
*Serikali yetu chini ya uongozi wa Rais wetu, Mhe Samia Suluhu Hassan
*Benki za NBC, NMB, CRDB na TPB
*Baadhi ya Wazaliwa wa Kata ya Kiriba

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 20.4.2022