RUWASA inaendelea kujenga miundombinu yenye ubora na sasa WANAKIJIJI wa CHITARE wameanza kupata maji safi na salama ya bomba.

Vijiji vya Chitare na Makojo vya Kata ya Makojo vimesubiri maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria tokea Mwaka 2013!

Mradi huu ulioanzwa kutekelezwa na Halmashauri yetu (Musoma DC) tokea Mwaka wa Fedha 2013/2014, sasa unarudiwa na unakamilishwa kwa ubora mzuri na RUWASA.

RUWASA inaendelea kujenga miundombinu yenye ubora na sasa WANAKIJIJI wa CHITARE wameanza kupata maji safi na salama ya bomba.

Kwa muda mfupi ujao Wanakijiji wa Makojo nao watapata maji ya bomba hilo.

Tumeomba bomba hilo lijengwe hadi Kijiji cha Chimati ambacho nacho kiko ndani ya Kata ya Makojo. Serikali imepokea ombi letu na kukubali kulitekeleza.

RUWASA inaendelea kufanya kazi zenye ubora mzuri ndani ya Jimbo letu.

FURAHA & SHUKRANI nyingi kutoka Kijiji cha Chitare zimeambatanishwa hapa – Sikiliza Clip/Video kutoka Chitare.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz