SEKONDARI ZA KATA ZAENDELEA KUJENGA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI

Ujenzi wa Maabara 3 (Physics, Chemistry & Biology) za Mtiro Sekondari ya Kata ya Bukumi, Musoma Vijijini.

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 lina Sekondari za Kata 25 na za Binafsi 2.

Jimbo hili limeamua kujenga Maabara 3 za Masomo ya Sayansi kwenye kila Sekondari ya Kata. Maabara hizo ni za Physics, Chemistry & Biology.

Sekondari 3 tu kati ya 25 ndizo zina maabara 3, nyingine zinazo mbili au moja.

Sekondari mpya zinazoendelea kujengwa na Wanavijiji lazima ziwe na maabara hizo.

Kwa hiyo, Fedha zote za Mfuko wa Jimbo, zinatumika kwenye ujenzi wa maabara hizo.

MTIRO SEKONDARI
*Sekondari ya Kata ya Bukumi yenye Vijiji 4 (Buira, Bukumi, Buraga & Busekera)
*Ilifunguliwa Mwaka 2006
Haina maabara hata moja

WANAFUNZI WA MTIRO SEKONDARI
*Jumla ya Wanafunzi ni 681
*Jumla ya Walimu wa ajira ya Serikali ni 13, na 4 ni Walimu wa muda (kujitolea) wanaopewa posho kutoka kwa Wazazi wenye watoto shuleni hapo.

Mwitikio wa Masomo ya Sayansi
*Walimu wanaofundisha Masomo ya Sayansi ni wanne (4)
*Walimu wanaofundisha Hisabati (Maths) ni wawili (2)

Jumla ya Wanafunzi wa Form III ni 110
*14 wanasoma Physics
*17 wanasoma Chemistry
*110 wanasoma Biology (kwa kulazimika)

Jumla ya Wanafunzi wa Form IV ni 123
*21 wanasoma Physics
*26 wanasoma Chemistry
*123 wanasoma Biology (kwa kulazimika)

UMUHIMU WA KUWEPO MAABARA KWENYE SEKONDARI
*Takwimu hizo hapo juu zinaonesha mwitikio mdogo sana wa wanafunzi wetu kupenda kusoma Masomo ya Sayansi

*Kuwepo kwa Maabara za Masomo ya Sayansi ni muhimu kwa kufundishia (Walimu) na kwa kujifunza, hasa kwa vitendo (Wanafunzi)

MTIRO SEKONDARI WANAJENGA MAABARA 3 ZA MASOMO YA SAYANSI

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, alipiga Harambee ya ujenzi wa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi, na matokeo ni MICHANGO ifuatayo:

Wanavijiji wa Vijiji 4
(michango inaendelea kutolewa)
*Nguvukazi ya kuchimba misingi
*Mchanga trip 27
*Kokoto trip 2
*Saruji Mifuko 8
*Fedha taslimu Tsh 1,508,000
*Wazaliwa wa Kata ya Bukumi & Wadau wengine
Tsh 1,500,000

Mbunge wa Jimbo
*Saruji Mifuko 150 (ameanza kwa kutoa 75)

Mfuko wa Jimbo
(Mwenyekiti, Mbunge wa Jimbo)
*Saruji Mifuko 200
*Nondo 49

MAOMBI KUTOKA KWA WANANCHI WA MUSOMA VIJIJINI
Halmashauri yetu (Musoma DC) ianze kuchangia ujenzi wa Maabara za Masomo ya Sayasi kwenye Sekondari zake za Kata, isusibiri kufanya kazi ya kuratibu fedha zinazotolewa na Serikali Kuu!

*Wazaliwa wa Musoma Vijijini waanze au waendelee kuchangia Sekondari za Kata za kwao kwenye ujenzi wa Maabara za Masomo ya Sayansi, na Maktaba.

SAYANSI NI KILA KITU

UCHUMI WA KISASA UNAHITAJI SAYANSI

MAFANIKIO MAKUBWA YA KIUCHUMI YA CHINA, INDIA & BRAZIL YANAENDANA NA UWEKEZAJI MKUBWA KWENYE SAYANSI

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatatu, 24.4.2023