Uzio unajengwa kwa kuhakikisha kwamba makaburi yaliyoko nje kidogo ya eneo la mpaka wa makaburi yanaingizwa ndani.
Makaburi yaliyo kwenye eneo la Kanisa la Mennonite la Kitaji, Musoma Mjini yalikuwa hayana uzio (ukuta). Utunzaji wake ni mgumu sana!
Wazo la kujenga uzio kwenye makaburi hayo lilitolewa na Profesa Sospeter Muhongo. Michango ilikaribishwa na kutolewa kwa kusuasua sana, na ikawa ni midogo mno! Michango ilipelekwa kwenye Kanisa lenye makaburi. Ujenzi ukaanza kwa kusuasua sana. Malumbano yakaanza kujitokeza.
Mtoa wazo la ujenzi, Prof Muhongo akaamua yafuatayo:
*Michango isimame, tuepuke malumbano.
*Ujenzi uendelee kwa ufadhili wake, yaani wa Prof Sospeter Muhongo
Maendeleo ya ujenzi:
*Eneo lenye makaburi limesafishwa kwa kukata nyasi na vichaka.
*Mafundi wengine wamewekwa kufanya kazi ya ujenzi.
*Uzio unajengwa kwa kuhakikisha kwamba makaburi yaliyoko nje kidogo ya eneo la mpaka wa makaburi yanaingizwa ndani. Angalia picha.
Nawatakia Jumapili njema
Sospeter Muhongo
Jumapili, 23.7.2023