Leo (21.3.2024) ni siku ya Umoja wa Mataifa (UN) ya kukumbushana umuhimu wa misitu ya aina zote.
UN ilipitisha azimio la siku hii (tarehe 21 Machi ya kila mwaka) kwenye Mkutano wake wa tarehe 28.11.2013
Kaulimbiu 2024: Misitu na Ubunifu
(Forests and Innovations)
Jimbo la Musoma Vijijini: Misitu na Ubunifu
Kwa muda wa zaidi ya wiki mbili, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt Khalfany Haule, na Meneja wa Misitu (TFS) Wilaya, Ndugu Boniphace Kaberege wamekuwa wakigawa na kupanda mamia ya miche ya miti ya matunda, mbao na kivuli kwenye shule kadhaa za misingi na sekondari za Jimboni mwetu. Kampeni hii ni endelevu!
Sherehe ya Uzinduzi wa Upandaji miti
Jana, TFS Wilaya chini ya uongozi wa Ndugu Boniphace Kaberege ilitoa mafunzo ya umuhimu wa misitu kwa maisha na ustawi wa jamii zetu. Mafunzo hayo yalifanywa kwenye Sekondari ya Suguti.
Wanafunzi na Walimu wote wa Sekondari hiyo, wakiongozwa na Mkuu wao, Mwl Pendo Kaponoke walihudhuria mafunzo hayo.
Wanavijiji wa Kata ya Suguti (Vijiji 4 vya Chirorwe, Kusenyi, Suguti na Wanyere) walihudhuria, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Ndugu Alphonce Wambura
"Environmental Ambassadors" - Suguti Sekondari:
Wanufunzi 100 wa Sekondari hii wamekuwa, Mabalozi wa Mazingira chini ya Mwalimu wao wa Mazingira, Mwl Keneth Elias. Hawa wataongoza Kampeni ya upandaji na utunzaji miti ndani ya Kata na Suguti, na kwingineko Jimboni mwetu.
Uzinduzi wa Upandaji na Utunzaji miti kwenye shule zote za Jimboni mwetu
Jana, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Meneja wa TFS Wilaya walizindua kampeni endelevu ya upandaji na utunzaji wa miti kwenye shule zote za Jimboni mwetu. Uzinduzi huo ulifanyika Suguti Sekondari.
Picha za hapa zinaonesha:
Matukio mbalimbali yaliyoelezwa hapo juu. Hapo ni Suguti Sekondari, Kijijini Suguti, Kata ya Suguti, Musoma Vijijini.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
The UN International Year of Forests
Tarehe:
Alhamisi, 21.3.2024