Kata ya Musanja yenye vijiji vitatu (3) haina Kituo cha Afya na haina Zahanati hata moja kwenye vijiji vyake. Vijiji hivyo ni: Mabuimerafuru, Musanja na Nyabaengere.
Hii ndiyo Kata pekee Jimboni mwetu yenye hali kama hiyo kwa upande wa Huduma za Afya!
Wanavijiji wa Kata hii wanalazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita kumi (km 10) kwenda kupata Huduma za Afya kwenye Kata jirani ya Murangi (Kituo cha Afya cha Murangi).
Zahanati ya Kijiji cha Nyabaengere:
Zahanati hii inakaribia kuanza kutoa Huduma za Afya. Maombi ya kufungiwa umeme yamepelekwa TANESCO.
Zahanati ya Kijiji cha Mabuimerafuru:
Mbunge wa Jimbo la MusomaVijijini, Prof Sospeter Muhongo aliendesha Harambee ya ujenzi wa Zahanati ya kijiji hiki siku ya Jumatano, 20.3.2024.
Matokeo ya Harambee hiyo:
1. Fedha zilizopatikana: Tsh 1,350,000
2. Saruji Mifuko 59
3. Kondoo 2
4. Mbunge wa Jimbo: Saruji Mifuko 200 (mia mbili)
Kamati ya ujenzi iliundwa chini ya uongozi wa Ndugu Justine Joshua
Michango kutoka kwa Wadau wa Maendeleo wa Kata ya Musanja:
Uchangiaji ufanyike kwa kutuma fedha za michango moja kwa moja kwenye Akaunti ya Kijiji ambayo ni:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30310037402
Jina: Kijiji cha Mabuimerafuru
Picha inaoneshaHarambee ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mabuimerafuru.
Viongozi wa CCM wa Kata na Matawi, na baadhi ya wananchi wa Kata ya Musanja walipewa vitabu viwili viwili vinavyoelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 ndani ya vijiji vyote 68 vya Jimboni mwetu.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumamosi, 23.3.2024