ETARO SEKONDARI INAJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU INAYOHITAJIKA KUANZISHA “HIGH SCHOOL” YA MASOMO YA SAYANSI

Idadi ya shule ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye jumla ya vijiji 68 ni kama ifuatavyo:

*Shule za Msingi 120: 116 (Serikali) na 4 (Binafsi). Shule Shikizi 13 (ujenzi unaendelea)

*Sekondari 28: 26 (Kata/Serikali) na 2 (Binafsi). 10 mpya (zinajengwa na wanavijiji)

Etaro Sekondari:
Ilifunguliwa Mwaka 2006, ina jumla ya wanafunzi 897 kutoka vijiji vinne vya Kata ya Etaro.

Maabara za Kemia & Baiolojia:
Sekondari hii inazo MAABARA MBILI zilizokamilika na zinatumika. Hizo ni maabara za masomo ya Kemia na Baiolojia.

Maabara ya Fizikia:
Maabara ya Fizikia (boma lipo) itakamilishwa ifikapo tarehe 30.4.2024 kwa kutumia vifaa vilivyonunuliwa kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini. Mbunge wa Jimbo ameikabadhi sekondari hiyo MABATI ya RANGI 120, SARUJI MIFUKO 100 na NONDO 40 kwa ajili ya ukamilishaji wa Maabara hiyo.

Chumba cha Kompyuta:
Kompyuta ishirini na tano (25) zimenunuliwa na rafiki wa Etaro Sekondari ambae ni Northern Illinois University, USA. Chuo hiki kilianzishwa tarehe 22.5.1895

Lengo la kuanzisha "high school" ya sayansi
Kwenye kikao cha hivi karibuni cha Mbunge wa Jimbo na wananchi wa Kata ya Etaro, moja ya maazimio muhimu yaliyofanyika ni uanzishwaji wa "high school" ya masomo ya sayansi, yakiwemo ya "computer science" kwenye sekondari hii.

Imepangwa kwamba Mwezi Julai 2024, Mbunge wa Jimbo ataendesha Harambee ya ujenzi wa mabweni, bwalo la chakula, n.k. ikiwa ni baadhi ya miundombinu muhimu inayohitajika kwa ajili ya uanzishwaji wa "high school"

PONGEZI:
Serikali yetu inapongezwa kwa kutoa michango mbalimbali ya ustawi wa Etaro Sekondari tokea Mwaka 2006

Wananchi wa Kata ya Etaro, hasa wazazi wa wanafunzi wa Etaro Sekondari wanapongezwa sana kwa kukubali kwao kuendelea kuchangia maendeleo ya sekondari yao.

Walimu, chini ya uongozi mzuri wa Mkuu wa Shule, Mwl Jacob Joseph Chagavalye wanapongezwa sana kwa ubunifu wao.

Rafiki zetu wa Marekani, Northern Illinois University nao wanapongezwa sana kwa uwezeshaji wao wa kutupatia na kutufungia mtando wenye Kompyuta 25 hapo shuleni.

Picha zetu zinaonesha:
Wanafunzi wa Etaro Sekondari wakiwa kwenye masomo ya vitendo (practicals) ndani ya Maabara ya Kemia na Chumba cha Kompyuta.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini akikabidhi vifaa vya ujenzi vya kukamilisha Maabara ya Fizikia ya Etaro Sekondari.

Vilevile, Mbunge huyo aligawa vitabu viwili (Volumes III & IV) vinavyoelezea mafanikio makubwa yanayopatikana Jimboni mwetu kutokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025.

TUENDELEE KUCHANGIA UBORESHAJI NA UPANUZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SHULE ZETU ZA MUSOMA VIJIJINI

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Ijumaa, 5.4.2024