Mvua zinaendelea kunyesha, na maji Ziwa Victoria yanaendelea kuongezeka.
Siku ya leo siyo nzuri Kisiwani Rukuba, Kaya ya Etaro kwani kaya tano (5) hazina makazi zimehifadhiwa kwenye Kituo cha Afya cha hapo Kisiwani. Maji yanaendelea kuongezeka, na makazi ya kaya nyingine thelathini na mbili (32) yako hatarini.
Kuongezeka kwa maji ndani ya Ziwa Victoria
Mifano hii miwili itatuonyesha jinsi maji yalivyoongezeka ndani ya Ziwa Victoria kwa upande wa Wilaya ya Musoma:
(i) Kisiwani Rukuba, Kata ya Etaro:
Waathirika wa Kisiwani humo wanasema, "maji yamewafuata" kwa takribani mita 30-40 hadi kwenye makazi yao
(ii) Mji wa Musoma:
Waathirika wanaoishi karibu na ufukwe wa Ziwa Victoria wanasema "maji yamewafuata kwa takribani mita 5" hadi kwenye makazi yao
Picha mbili kutoka Mtaa wa Ziwa (Lakeside street) zimeambatanishwa hapa - picha zenya magugu maji (water hyacinth)
(iii) Ofisi ya Bonde la Ziwa Victoria, Mwanza:
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amewasiliana na wataalamu wetu walioko kwenye Ofisi hiyo, na kupata jibu lifuatalo:
maji yameongezeka kwa kiasi cha
wastani wa kina cha mita 1.65
USHAURI:
Wananchi wanaoishi karibu na ufukwe wa Ziwa Victoria wanalazimika kufuata ushauri watakaopewa na viongozi mbalimbali, kwa ajili ya kuepuka mafuriko au ongezeko la maji ndani ya Ziwa Victoria.
Vilevile, wananchi wanahimizwa kufuatilia utabiri wa hali ya hewa unaotolewa kila siku na wataalamu wa hali ya hewa wa TMA.
Ziwa Victoria lenye kawaida ya ujazo wa maji wa takribani kilomita za ujazo 2,424 (2,424 cubic kilometres), kwa sasa maji yaongezeka sana! Tuchukue tahadhari kubwa!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumamosi, 4.5.2024