UCHUMI MKUBWA WA MUSOMA VIJIJINI KUTOKA NDANI YA ZIWA VICTORIA: UVUVI WA VIZIMBA

Ziwa Victoria lina umri wa takribani miaka 400,000 na ujazo wake wa kawaida ni kilomita za ujazo 2,760 (2,760 cubic kilometres).

Mvua za mwaka jana ziliongeza ujazo wa maji ndani ya bonde la Ziwa Victoria lenye ukubwa kilomita za miraba 195,000 (195,000 square kilometres). Lilikuwa ongezeko la kina cha takribani mita 1.7 (ca. 1.7 meters depth)

Ziwa Victoria ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini:

Kata 18 kati ya Kata 21 za Jimbo letu zina ufukwe wa Ziwa Victoria. Kwa hiyo, asilimia 85.7 (85.7%) za Kata zetu zina fursa nzuri za kutumia raslimali za maji ya Ziwa hili.

Samaki wamepungua sana ndani ya Ziwa Victoria na mito inayolizunguka. Suluhisho la tatizo hili ni kuanzisha na kuendeleza uvuvi wa ufugaji wa samaki ziwani humo (aquaculture fish farming)

Upungufu wa samaki haupo tu ndani ya Ziwa Victoria, bali ni tatizo kubwa ulimwenguni kote! Bahari, maziwa na mito ya Duniani kote ina upungufu mkubwa wa samaki.

Kwa hiyo, kwa sasa takribani nusu (ca. 50%) ya samaki Duniani kote wanapatikana kupitia ufugaji wa samaki ndani ya bahari, maziwa, n.k. (aquaculture fish farming)

Uvuvi wa Vizimba Musoma Vijijini:

Malengo:
(i) Kata 18 kati ya 21 za Jimboni mwetu kuanzisha na kuendeleza Uvuvi wa Vizimba ndani ya Ziwa Victoria

(ii) Mitaji ya Uvuvi wa Vizimba kupatikana kutoka:
(iia) Mitaji ya watu binafsi: vizimba 10 vimeishaanza uzalishaji
(iib) Mitaji kutoka mikopo nafuu ya Serikali Kuu: vizimba 8 tayari vimetayarishwa na kuwekwa Ziwani. Uzalishaji utaanza ndani ya miezi 3 ijayo
(iic) Mitaji kutoka mikopo mizuri ya Benki za Biashara (CRDB & NMB). Mikopo 10 ya vizimba 50 itatolewa hivi karibuni.

Mafanikio ya awali ya Uvuvi wa Vizimba:

Baadhi ya wavuvi wa vizimba wa Musoma Vijijini wamemueleza Mbunge wao wa Jimbo kwamba, kwenye kizimba kimoja chenye kipenyo cha mita 10 (10m-diameter) wamefanikiwa kuvuna tani 12 za samaki wenye thamani ya Tsh milioni 100 (Tsh 100m)

UVUVI WA VIZIMBA KUKUZA KWA KASI KUBWA UCHUMI WA MUSOMA VIJIJINI - Karibuni kwenye uvuvi wa kisasa ndani ya Ziwa Victoria!

Video/Clip zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
Vizimba vikiwa ndani ya Ziwa Victoria kwenye eneo la Jimbo la Musoma Vijijini

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatatu, 17 Feb 2025