TUENDELEE KUKUMBUSHANA – UJENZI WA SEKONDARI MPYA VIJIJINI MWETU

Jimbo la Musoma Vijijini lenye jumla ya Kata 21 lina:
*Sekondari 26 za Kata/Serikali
*Sekondari 2 za Madhehebu ya Dini

I - Sekondari 3 zinazojengwa na Serikali Kuu
(ujenzi kukamilika: 28 Feb 2025)

(i) Kijijini Butata, Kata ya Bukima
(ii) Kijijini Kasoma, Kata ya Nyamrandirira
(iii) Kijijini Kurwaki, Kata ya Mugango

Wanavijiji wamekubali kuchangia nguvukazi zao kwenye ujenzi wa sekondari hizo

II-Sekondari 9 zinajengwa kwa kutumia nguvukazi na michango ya fedha kutoka kwa wanavijiji, wazaliwa wa vijiji vyenye ujenzi na viongozi wao

(iv) Kijiji cha Muhoji, Kata ya Bugwema
(itafunguliwa 28 Feb 2025)
(v) Kisiwa cha Rukuba, Kata ya Etaro
(vi) Kijiji cha Mmahare, Kata ya Etaro
(vii) Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifu
(viii) Kijiji cha Kiriba, Kata ya Kiriba
(ix) Kijiji cha Kataryo, Kata ya Tegeruka
(x) Kijiji cha Musanja, Kata ya Musanja
(xi) Kijiji cha Chitare, Kata ya Makojo
(xii) Kijiji cha Nyambono, Kata ya Nyambono

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:

1. Picha yenye mapipa: Wanakijiji wa Chitare, Kata ya Makojo wakiwa wanafyatua matofali ya ujenzi wa Chitare Sekondari. Hii sekondari ya pili ya Kata hii.

2. Wanakijiji wa Mmahare, Kata ya Etaro wakiwa wanafyatua matofali ya ujenzi wa Mmahare Sekondari. Hii ni sekondari ya tatu ya Kata hii.

KARIBUNI TUCHANGIE UJENZI WA SHULE MPYA ZA MSINGI NA SEKONDARI JIMBONI MWETU

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumanne, 18 Feb 2025