Mwanzo-en

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

"Tovuti Rasmi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo, Kwaajili ya Kuwasiliana na Wananchi Jimboni "

KUHUSU SISI : Utawala | Mbunge |Sheria

MBUNGE WETU MH. PROF. SOSPETER MUHONGO ANATUHAMASISHA KUTEMBELEA WEBSITE HII KILA MARA, KWA MAENDELEO YETU SOTE.

Matukio katika picha - (Toa Maoni Hapa)

Habari Mpya Toka Jimboni

HUDUMA ZA BENKI ZAANZA KUSHAMIRI VIJIJINI MWETU

Benki za CRDB na NMB tayari zina MAWAKALA wanaotoa HUDUMA ndani ya VIJIJI vyetu. Hii ni hatua muhimu kabla ya ujenzi wa MATAWI ya BENKI hizo JIMBONI mwetu.
NMB - MAWAKALA
*Bukima (2) na Mugango
CRDB - MAWAKALA
*Bukima, Mugango Saragana na Seka
NBC - itaanzia Murangi
MAWAKALA WAJAO:
CRDB (Bwai Paris), NMB (Busekela, Bwai Paris, Etaro, Nyambono na Seka)

UJENZI WA OFISI YA CCM (W) KIJIJINI MURANGI

MICHANGO ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter  Muhongo YAFIKIA Tsh MILIONI 12.
Mchanganuo ni huu:
(i) Tsh Milion 6 kulipia gharama za ujenzi (FUNDI).
(ii) Ununuzi wa Saruji Mifuko 200
(iii) Kulipia gharama za ufyatuaji na umwagiliaji wa  matofali ya Mifuko 200.
KAMATI YA UJENZI itasimamia ujenzi huu (Mwenyekiti: DC Musoma District)

Kalamu ya Mh. Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo

KUONGEZA HIGH SCHOOLS MUSOMA VIJIJINI

* Tunazo High Schools 2 (Kasoma- Serikali na Nyegina-Katoliki)
* Halmashauri imeamua kuboresha baadhi ya Sekondari zetu  ziwe na High Schools. Sekondari hizo ni:
(1) Bugwema, (2) Mtiro, (3) Mugango na (4) Mkirira
* Bwasi Sekondari (SDA) imeombwa ianzishe High School.
Tunazo Sekondari 20 (Serikali) na 2 (Binafsi). Tunajenga MPYA 5, na nyingine zitajengwa. Tuanze KUONGEZA HIGH SCHOOLS.
Ofisi ya Mbunge
7.6.2020

MAOMBI YA UMEME WA REA

Mbunge wa Jimbo amewasiliana na REA & TANESCO kwa kusudio la kuongeza kasi ya USAMBAZAJI WA UMEME WA REA Vijijini mwetu.
LETA MAOMBI:
yakitaja MTAA,  KITONGOJI na KIJIJI ambacho hakijapata UMEME
TAARIFA zipelekwe OFISI ya MBUNGE:
Fedson:
0623 608 686
Hamisa:
0762 626 881
Verediana:
0763 503 033
Jumatatu, 8 Mei 2020, MBUNGE wa Jimbo atawasiliana na REA kuhusu MAOMBI yetu.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

TUMEANZA UJENZI WA WODI ZA MAMA NA MTOTO 

ZAHANATI za VIJIJI vya BUKIMA, NYEGINA na RUKUBA KISIWANI zinajenga WADI hizo.
MICHANGO ya UJENZI inatoka kwa WANAVIJIJI, HALMASHAURI yetu na MBUNGE wa Jimbo
Mbunge wetu, Prof Sospeter Muhongo ameanza kuchangia na atatoa SARUJI MIFUKO 200 kwa kila ZAHANATI (jumla atachangia Mifuko 600). SARUJI ya MBUNGE inatolewa kulingana na KASI YA UJENZI.

Matukio Mbalimbali Jimboni

Vipaumbele vya Mh. Mbunge

Elimu

Kila mtoto aliyefikia umri wa kwenda shule, awe shuleni na kuinua kiwango cha ufaulu

Afya

Kusogeza huduma bora za afya zinazokidhi uhitaji kwa wananchi

Kilimo

Kilimo cha kisasa, endelevu na chenye uzalishaji mkubwa kwa eneo

Maji

Gharama nafuu katika upatikanaji wa maji safi na salama kwa kila kaya