Na Hamisa Gamba, Msaidizi wa Mbunge
Tarehe 23.10.2018
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo amechangia Saruji Mifuko 50 iliyokabidhiwa na Msaidizi wake kwenye Harambee iliyoendeshwa ili kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa Jengo la Utawala wa Shule ya Sekondari Suguti. Haya yalifanyika tarehe 19.10.2018, siku ya Mahafari ya 10 ya Kidato cha IV shuleni hapo.
Awali, akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Suguti, Ndugu Pendo Kaponoke alitaja changamoto zinazoikabili Sekondari hiyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa Maktaba, Maabara, Nyumba za Waalimu za kukidhi mahitaji na Jengo la Utawala.
Akitoa Hotuba kwenye Mahafali hiyo, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Musoma, aliyewakilishwa na Ndugu Raymond Romuli ambae ni Katibu Tarafa, aliwaasa Wahitimu, na Wanafunzi wote kutilia mkazo Elimu, na kufanya kwa umakini mitihani yao, na kuwa waadilifu sehemu yoyote wawapo.
Mgeni Rasmi alichangia Tsh 300,000/= ili kufanikisha ujenzi wa Jengo la Utawala huku akiwahamasisha WAZAZI na JAMII kujituma zaidi katika kushiriki na kuchangia shughuli za maendeleo.
Msaidizi wa Mbunge, akiongea kwa niaba ya Mbunge, aliwahimiza Wanafunzi wote kuzingatia sana Elimu kwa kufanya mitihani yao vizuri ili kupata matokeo mazuri. Pia aliwaomba Wazazi wajitume kwa hali na mali kushiriki katika shughuli za Maendeleo kwenye Sekta za Elimu, Afya na Kilimo.
Saruji Mifuko 50 iliyotolewa na Mbunge Prof Muhongo itatumiwa kukamilisha Jengo la Utawala wa Sekondari hii.
Kwa siku za nyuma Mbunge Prof Muhongo alishatoa misaada ya VITABU, MADAWATI, MBEGU ZA ALIZETI, SARUJI MIFUKO 50, n.k kwenye Shule ya Sekondari Suguti.
NDUGU ZANGU WA MUSOMA VIJIJINI – MATOKEO YA MITIHANI YA SHULE ZETU ZA MSINGI NI MABAYA…. naomba tujikumbushe:
(1) “Education comes from within; you get it by struggle and effort and thought.” Napoleon Hill (1883-1970).
(2) “An investment in knowledge pays the best interest.” President Benjamin Franklin (1706-1790)
KARIBUNI TUCHANGIE UBORA WA ELIMU MUSOMA VIJIJINI