Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Buira, Kata ya Bukumi wamejenga MAKTABA kwenye S/M Buira. Uezekaji wake utafanyika wiki ijayo.
Leo, Jumatano, tarehe 02.01.2019 Kijiji cha Buira KIMEPOKEA MREJESHO WA 20% ya Makusanyo yake kutoka kwenye Mwalo wa Buira. Hizi ni takribani Sh Milioni 6. PONGEZI ZA DHATI ZINATOLEWA KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI, Ndugu John Kayombo na Halmashauri yote kwa kuwezesha fedha hizo kupatikana na kurudishwa Kijijini Buira (kupitia Benki).
Sehemu ya fedha hizo imenunua Mabati 57, Saruji Mifuko 20, Mbao na Misumari kwa ajili ya KUEZEKEA: (a) Vyumba vya Madarasa 2, (b) Ofisi ya Walimu,1 na (c) Maktaba 1.
Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo AMETIMIZA AHADI YAKE leo (02.01.2019) kwa kununua MABATI 54 kwa ajili ya ujenzi huo kwenye S/M Buira.
Vilevile Mbunge Prof Muhongo AMEHAIDI KUIGAWIA VITABU Maktaba Mpya hiyo kutoka kwenye Kontena la Vitabu kutoka USA ambavyo bado hajaanza kuvigawa Jimboni. Shule zote za Msingi na Sekondari ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini zimeishagawiwa mara tatu VITABU kutoka USA na UK.
Wananchi na Viongozi kwenye Vijiji vyote 68 WAMEAMUA kutatua TATIZO SUGU la UPUNGUFU wa Vyumba vya Madarasa kwenye Shule za Msingi 112 (ikiwemo 1 ya binafsi) na Sekondari 20 (zikiwemo 2 za binafsi).
JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – HATUTAKI BAADHI YA WANAFUNZI WAENDELEE KUSOMEA CHINI YA MITI au WABANANE MADARASANI – TUTAFANIKIWA, TUJITUME KWA VITENDO!