Alhamisi, 30.05.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
*Ujenzi wa Sekondari hiyo ya Kata ya Bugoji ulianza Disemba 2018
MALENGO:
(1) Ifikapo tarehe 01 Agosti 2019 MAJENGO yanayohitajika Sekondari KUSAJILIWA na Serikali yawe yamekamilika.
(2) January 2020 Wanafunzi wa Form I waanze MASOMO yao hapo. Wengi wao watatoka kwenye Kata ya Bugoji yenye Vijiji 3 – Kanderema, Kaburabura na Bugoji.
WACHANGIAJI wa UJENZI wa Sekondari hii kupitia HARAMBEE za Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ni:
A- WANANCHI wa Vijiji 3 vya Bugoji, Kanderema na Kaburabura. Wanasomba maji, mchanga, mawe na kokoto. Vilevile wanachangia Fedha Taslimu – Tsh 17,000 kutoka kila KAYA. Wanalipa MAFUNDI ujenzi.
B-WAZALIWA wa Kata ya Bugoji na WADAU wengine wa Maendeleo wakiongozwa na Diwani wa Kata Mhe Ibrahimund Malima. Wengine ni:
Mkwaya Toto, Musyangi Kaitira, Chiguti Mwesa, Petro Mufungo, Mafuru Kaitira, Munepo Machumu, Palapala Burenga, Martha Antoni, Mwalimu Morelia, Mwalimu Onesimo, Ndugu Nashoni, Raphael Magoti, Sostenes Ruhumbika, Alfred Majani, Evarist Maganga
C- FAMILIA ya Marehemu Jaji Dan Petro Mapigano
D-MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini
E- MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo
SHEREHE za uwekaji wa Jiwe la Msingi la Dan Mapigano Memorial Secondary School zilifanywa tarehe 22.04.2019 Gharama za Sherehe hizo zilibebwa na Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo, Diwani wa Kata, Mhe Ibrahimund Malima na Viongozi wengine wa Kata na Vijiji.
MIPANGILIO YA UJENZI NA MAFANIKIO YAKE
(i) Ujenzi wa Vyumba 5 vya Madarasa na Ofisi 2 za Walimu UMEKAMILIKA. Angalia picha hapo chini.
(b) HALMASHAURI inasubiriwa ikamilishe MICHORO ya MAABARA (zitajengwa wa Kijiji cha Kanderema), Vyumba vingine 3 vya Madarasa (vitajengwa na Kijiji cha Bugoji) na Nyumba ya Walimu (itajengwa na Kijiji cha Kaburabura).