04.06.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
SERIKALI yetu imetoa Tsh Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Hospital hiyo inajengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti, Kata ya Suguti.
WANANCHI wa Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji vyote 374 vya Jimbo la Musoma Vijijini WAMEKUBALI KUCHANGIA ujenzi huu kwa Kila KATA kuchangia Tsh Milioni 7.5. MADIWANI na WATENDAJI wa Kata na Vijiji wanasimamia UKUSANYAJI wa MICHANGO hiyo. Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ataungana na WANANCHI na SERIKALI kuchangia ujenzi huo.
Jana, Jumatatu, 03.06.2019 Mbunge wa Jimbo akifuatana na VIONGOZI wa CCM Wilaya (M/Kiti WAZAZI, Katibu, Ma-Katibu wa Jumuiya za Chama- UWT, WAZAZI na UVCCM) WALIKAGUA UJENZI wa Hospitali hiyo ya Wilaya.
MAJENGO 8 yanayojengwa kwa sasa ni:
(1) Jengo la Utawala: Linakamilishwa usawa wa lenta
(2) Jengo la Mapokezi (OPD): Lipo hatua ya kumwaga Jamvi
(3) Jengo la Maabara: Boma limekamilika tayari kwa kuezekwa
(4) Jengo la Mionzi (Radiology): Lipo hatua ya kumwaga Jamvi
(5) Jengo la Mama na Mtoto: Lipo hatua ya kumwaga Jamvi
(6) Jengo la Ufuaji (Laundry): Lipo hatua ya kumwaga Jamvi
(7) Jengo la Madawa (Pharmacy): Lunamwagwa Jamvi
(8) Jengo la Kichomea Taka: Lipo hatua ya Msingi
Mkuu wa Wilaya (DC) Dr Vicent Naayo Anney na Mkurugenzi wa Halmashauri (DED) Ndugu John Kayombo WANASIMAMIA ujenzi huu kwa UBUNIFU na UFANISI mkubwa.