SHEREHE NA MAENDELEO VIJIJINI: KATA YA KIRIBA IMEANZA UJENZI WA MIUNDOMBINU KWENYE SHULE ZAKE KWA KASI MPYA

MAABARA ya Kemia inavyoonekana kwa ndani , Mwalimu Mkuu (mwenye Bag begani) akitoa maelezo kuhusu maabara hiyo.

Alhamisi, 06.06.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
Kata ya Kiriba yenye Vijiji 3 vya Bwai Kwitururu, Bwai Kumusoma na Kiriba hapo siku za nyuma ILISHINDWA kutekeleza MIRADI ya MAENDELEO kwa kasi kubwa kwa sababu ya malumbano ya VIONGOZI.
VIONGOZI na WANANCHI sasa WAMEAMUA kuweka pembeni tofauti zao za kisiasa na KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA kwenye UTEKELEZAJI wa Miradi ya Maendeleo.
Leo, 06.06.2019 Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo, akifuatana na Katibu wa CCM Wilaya, Ndugu Stephen Koyo na Katibu wa UVCCM Wilaya, Ndugu Peter Kabwe WAMEKAGUA ujenzi wa Vyumba vya Madarasa, Maabara na Vyoo kwenye SEKONDARI ya KIRIBA na Shule za Msingi za Chanyauru A&B.
KIRIBA SECONDARY SCHOOL
Sekondari hii ya Kata ilianzishwa Mwaka 2006. Kwa sasa ina Wanafunzi 686, Walimu 21 (Walimu wa Masomo ya Sayansi 6, mmoja akiwa wa kujitolea).
VYUMBA VYA MADARASA – KIRIBA SECONDARY SCHOOL
Sekondari hii ina Vyumba vya Madarasa 16 na vingine 4 vinajengwa ambavyo vitaanza kutumika kuanzia tarehe 08.07.2019.
Wastani wa WANAFUNZI kwenye  Chumba 1 cha Darasa ni 50-60. Vyumba vipya 3 vikianza kutumika tarehe 08.07.2019, WASTANI wa Wanafunzi kwenye Chumba 1 cha Darasa itakuwa 40-45.
Mwaka jana (2018), Wanafunzi waliomaliza Kidato cha 4 walikuwa 73 na kati ya hao 11 wameendelea na Masomo ya Kidato cha V na 6 wamejiunga na Vyuo mbalimbali.
WANANCHI wa Kata ya Kiriba WAMEKUBALI kuchangia Tsh 15,000 kwa kila KAYA kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa. NGUVUKAZI zao zinatumika kusomba mchanga, kokoto, mawe na maji.
SERIKALI kupitia MRADI wake na WAFADHILI wa EP4R imechangia Tsh Milioni 37.5 kwa ajili ya ujenzi huo.
HARAMBEE ya leo iliyofanyika hapo Sekondari IMEWEZESHA Wananchi kuchangia Tsh Milioni 807,000/= na Mbunge mwenyewe AMECHAGIA MABATI 54.
Mbunge wa Jimbo alishatoa VITABU zaidi 1,000 (elfu) kwenye Sekondari hii. Vilevile Mbunge huyu amekubali KUSHIRIKIANA na Wazazi na BODI ya Shule KUCHANGIA POSHO ya Mwalimu wa Kujitolea wa Masomo ya Sayansi kwa muda wa miaka 2.
UONGOZI wa Shule chini ya Mwalimu Mkuu Robertious Wanjara, UONGOZI wa Kata chini ya DIWANI Mhe Msendo Mgire na VIONGOZI mbalimbali wa Chama (CCM) WANAFANYA KAZI NZURI ya KUBORESHA UFAULU na UBORA wa Elimu itolewayo Kiriba Secondary School.
MAABARA – KIRIBA SECONDARY SCHOOL
Shule imekamilisha MAJENGO ya MAABARA 3 – Chemistry, Physics na Biology. Hatua inayofuata ni kujenga MIUNDOMBINU ya NDANI ya kila Maabara.
Walimu wa Masomo ya Chemistry, Physics na Biology WATASHIRIKIANA na MAFUNDI wa FANI mbalimbali kutayarisha BAJETI (gharama) za kazi hiyo. Kazi hii itakamilika Jumatatu, 10.06.2019. MICHANGO ITAHITAJIKA KUKAMILISHA MAABARA HIZO.