Jumapili, 09.06.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
Sherehe za Eid el Fitr za Mwaka huu (2019) zilifanyika ndani ya Jimbo letu kwenye MISIKITI 3 ya VIJIJI 3 vya Kome (Kata ya Bwasi), Mayani (Kata ya Tegeruka) na Nyegina (Kata ya Nyegina).
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ALIWAKARIBISHA Waislamu na Wanavijiji wa Madhehebu mengine kwenye Kifungua Kinywa cha Eid (Eid el Fitr Breakfast) na Chakula cha Mchana cha Eid (Eid el Fitr Lunch) kwenye MISIKITI hiyo 3.
Vilevile, Sikukuku hiyo ilitumika kukagua na kuchangia MIRADI ya MAENDELEO kwenye VIJIJI 3 vilivyokuwa WENYEJI wa Sikukuu hiyo kwa Mwaka huu.
KIJIJI CHA NYEGINA CHAAMUA KUJENGA SEKONDARI YAKE
Watoto wa Kijiji cha Nyegina wanatembea UMBALI MKUBWA wa kilomita 4-7 kwenda MASOMONI kwenye Sekondari ya Kata yao ya Nyegina (Mkirira Secondary School) iliyoko Kijiji jirani cha Mkirira.
Kutokana na TATIZO hilo la umbali mkubwa wa kutembea kwenda masomoni Sekondari ya Kata, Wakazi wa Kijiji cha Nyegina WAMEAMUA kujenga Sekondari yao, Kijijini mwao.
UJENZI umeanza kwa kutumia NGUVUKAZI za Wananchi wa Kijiji hicho – wanasomba mchanga, mawe, kokoto, maji na matofali yanayonunuliwa kutoka Kanisani Nyegina. Vilevile WANAKIJIJI hao wanachangia Fedha Taslim, Tsh 12,600 kwa kila KAYA kwa ajili ya ujenzi huo. Hayo yalisemwa na Diwani wa Kata hiyo, Mhe Rajabu Majira Mchele na Kaimu Mtendaji wa Kata, Ndugu Erick Mjema.
Hadi kufikia tarehe 05.06.2019, Boma la Vyumba vya Madarasa 2 na Ofisi 1 ya Walimu lilishajengwa likiwa tayari kuezekwa. Msingi wa Vyumba vingine 2 na Ofisi 1 ya Walimu ulikuwa umechimbwa na ujenzi wake unaendelea.
LENGO KUU – ifikapo Januari 2020, Wanakazi wa Kijiji cha Nyegina WANATAKA WATOTO wao waanze Elimu ya Sekondari (Form I) Kijijini mwao na kwenye Sekondari yao.
HARAMBEE YA MBUNGE WA JIMBO
MAHITAJI YA KUKAMILISHA MABOMA 4 NA OFISI 1 YA WALIMU
1. Saruji Mifuko 50
2. Matofari 3,500 (@Tsh 1,000)
3. Fundi Tsh 700,000/=
4. Nondo 30
MICHANGO ILIYOPATIKANA KUPITIA HARAMBEE hiyo:
1. Saruji Mifuko 47
2. Matofali 1,799 (Wananchi na Viongozi wao akiwemo Mhe Diwani Majira 799 na Mbunge wao 1,000)
*Mbali ya MCHANGO huo wa awali wa Matofali 1,000 (elfu moja), Mbunge wao Prof Muhongo AMEAHIDI kuendelea kuchangia hadi hapo Sekondari itakapokamilika.
WAZALIWA wa Kijiji cha Nyegina waishio nje ya Kijiji hicho wameanza kutoa MICHANGO yao kwa ajili ya ujenzi huu. Walioanza ni:
1. Robeta Masinde
2. Bahati Taraya
3. Shida Chogero
Picha hapo chini zinaonyesha Mbunge Prof Sospeter Muhongo akiwa na Wananchi wakiwemo Waumini wa Dini ya Kiislamu kwenye Msikiti wa Kijijini Nyegina (Eid el Fitr) na kwenye eneo la ujenzi wa Sekondari ya Kijiji cha Nyegina (Harambee ya ujenzi).
KARIBU TUCHANGIE MAENDELEO KWA VITENDO