Jumamosi, 22.06.2019
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
TAKWIMU
* Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374
*ZAHANATI za Serikali zinazotoa huduma: 23
*ZAHANATI za Binafsi zinazotoa huduma: 4
*ZAHANATI MPYA zinazojengwa na Wananchi: 13
*VITUO VYA AFYA vya Serikali vinavyotoa huduma: 2 (Murangi & Mugango)
* VITUO VY AFYA VIPYA vinavyojengwa na Wananchi: 1 (Nyambono)
*HOSPITALI YA WILAYA ya Serikali inayojengwa: 1 (Kitongoji cha Kwikonero, Kijiji cha Suguti)
* MAGARI ya Wagonjwa (AMBULANCES): 5 (tano) yalitolewa na Mbunge wa Jimbo, Prof Muhongo.
KITUO CHA AFYA CHA KATA YA NYAMBONO
Mnamo Disemba 2017, Wananchi wa Kata ya Nyambono (Vijiji 2: Nyambono na Saragana) walianza ujenzi wa Kituo chao cha Afya kinachojengwa katika Kijiji cha Nyambono.
Wananchi hao wamekubali kuendesha shughuli za ujenzi huo kwa KUJITOLEA kusomba maji, mawe, mchanga na kokoto. Vilevile WANACHANGIA Fedha Taslimu Tsh 11,000 (elfu kumi na moja) kutoka kila KAYA.
Sambamba na jitihada hizo za WANANCHI, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo ameungana na Wanavijiji hao kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 100 na NONDO 18.
WAZALIWA au wenye CHIMBUKO la Kijiji cha Nyambono ambao kwa sasa wanaishi nje ya Kijiji hicho ndio walioanzisha MRADI huu wa ujenzi. Wameanza kuchangia tangu hatua za Msingi na hadi sasa BOMA la OPD linapokaribia kukamilika. Wadau hawa wamekwishachangia Fedha taslimu jumla ya Tshs.5,954,000/= katika Mradi huu.
Aidha Uongozi wa Kijiji na Kata ya Nyambono, ukiongozwa na Diwani wa Kata ya Nyambono Mhe Mkoyongi Masatu Nyanjaba umetoa SHUKRANI za kipekee kwa WADAU WOTE wa Maendeleo wanaochangia ujenzi wa Kituo cha Afya Nyambono ambao ni: Wanavijiji, Wazaliwa wa Nyambono na Mbunge wa Jimbo, huku akibainisha kuwa ujenzi wa BOMA hilo la OPD utakamilika mapema wiki ijayo (picha hapo chini).
WANAVIJIJI na VIONGOZI wa Kata na Kijiji cha Nyambono wanaendelea KUTOA SHUKRANI nyingi na za dhati kwa WAZALIWA na wenye CHIMBUKO la Nyambono kwa MICHANGO yao. Wachangiaji hao ni:
1. Mkama Manyama
2. Nice Kuleba
3. Majura Songo
4. Eliud Kwabira
5. Shida Mulegi
6. Beredy Maregesi
7. Maganira Daudi
8. Malenya Sambu
9. David Alal
10. Bunyata Mkama
11. Adonias Mkama
12. Japhet Maganira
13. Mch. Yeremia Magomba
14. Ominde John
15. Albinus Manumbu
16. Benedict Mkama
17. Dickson Mufungo
18. Ching’oro Ebanda, na wengine wote wanaoendelea kutoa ushirikiano wao kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nyambono.
“OKOA MAISHA yako, ya NDUGU, JAMAA na WATANZANIA wengine kwa ujumla kwa KUCHANGIA ujenzi wa Kituo cha Afya Nyambono – KARIBU NAWE UCHANGIE ujenzi huu.”