KILIMO CHA UMWAGILIAJI CHANUFAISHA KIUCHUMI KIKUNDI CHA MKULIMA JEMBE CHA KATA YA BUKIMA

WANACHAMA wa Kikundi cha MKULIMA JEMBE wakiwa kwenye SHAMBA lao la MATIKITI, Kijijini Kastam, Kata ya Bukima.

Jumapili, 23.06.2019
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Kikundi cha MKULIMA JEMBE kilichopo Kijiji cha Kastam, Kata ya Bukima kilianzishwa Mwaka 2014  kikijishughulisha na uoteshaji wa MICHE badaye  walifanikiwa kuanzisha KILIMO cha UMWAGILIAJI wakilima MBOGAMBOGA, MATUNDA pamoja na mazao ya CHAKULA – viazi vitamu, maharage na mahindi.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Ndugu Festo Obed ameeleza kuwa  kupitia KILIMO cha UMWAGILIAJI  wamefanikiwa kununua Mashine/Pampu ya Umwagiliaji ya SOLAR, kusomesha Watoto wao na kujikimu kwenye matumizi mengine ya kifamilia. Fedha zao zinatunzwa Benki.
Ndugu Obed ameendelea na kusema kwamba, Kikundi cha MKULIMA JEMBE kimefanikia kuanzisha Kikundi kingine kiitwacho “TUMETAMBUA” ambacho kinajishughulisha na Kilimo cha Umwagiliaji na kina Mradi wa KUWEKA na KUKOPESHANA.
Afisa Kilimo wa Kata ya Bukima, Ndugu Mushangi Salige ameeleza kuwa Kata hiyo  ina fursa kubwa ya kupanua KILIMO cha UMWAGILIAJI kwa sababu Wakazi wengi wapo kando kando mwa Ziwa Viktoria.
Afisa Kilimo huyo amemshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwa kuwezesha Kikundi cha MKULIMA JEMBE kupata Vifaa vya Umwagiliaji (pampu na mipira) kutoka MFUKO wa JIMBO. Kikundi hicho na vingine Jimboni viligawiwa bure MBEGU za Mbogamboga na  Matunda.
Vilevile Wanavijiji wa Kata hiyo ya Bukima wanamshukuru sana Mbunge wao Prof Muhongo kwa KUWAGAWIA BURE Mbegu za ALIZETI, MTAMA na MIHOGO, amesema Afisa Kilimo huyo.