Wananchi wa Vijiji 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini WANATOA SHUKRANI ZA DHATI kwa Serikali yao kwa kuanza KUTEKELEZA MIRADI ya USAMBAZAJI wa MAJI SAFI na SALAMA Vijijini mwao.
(1) SHUKRANI MAALUM zimetolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Joseph Pombe Magufuli KWA KUTIMIZA AHADI YAKE ya KUTEKELEZA Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama. Maji yatatoka Ziwa Viktoria.
MRADI wa Mugango-Kiabakari-Butiama utagharimu Tsh bilioni 70 ( US$ 30.68) umefadhiliwa na Serikali ya Tanzania, Saudi Arabia na BADEA. Mradi huu utakamilika ndani ya MIEZI 24.
(2) MRADI WA MAZIWA MAKUU
Vijiji vyote vya Jimbo la Musoma Vijijini vilivyoko karibu na Ziwa Viktoria (Vijiji 33) vimo kwenye Mradi huu. USANIFU umefanyika na Serikali inajipanga ianze utekelezaji wake.
(3) MAJI YA MUWASA KUSAMBAZWA VIJIJINI
MAJI yanayozalishwa MUWASA kwa ajili ya Mji wa Musoma ni MENGI MNO na matumizi yake kwa sasa ni takribani 50% ya MAJI yanayozalishwa. Maji yanatoka Ziwa Viktoria.
Kwa hiyo Serikali imeamua Vijijini vya Jimbo la Musoma Vijijini na Jimbo la Butiama VISAMBAZIWE MAJI hayo ya ziada. Kwa upande wa Jimbo la Musoma Vijijini, VIJIJI VYOTE vya Kata za ETARO, NYEGINA, NYAKATENDE na IFULIFU vimo kwenye Mradi huu ambao UTEKELEZAJI wake tayari umeanza.
(4) MIRADI MINGINE INAYOTEKELEZWA na MAJI yake yanatoka Ziwa Viktoria ni:
(4a) Bujaga-Bulinga-Bukima-Kwikerege
(4b) Chitare-Makojo
(4c) Suguti-Kusenyi-Chirorwe-Wanyere
(5) MIRADI AMBAYO USANIFU UMEKAMILIKA
USANIFU kwenye VIJIJI vya Kata za Bugoji, Nyambono, Bugwema, Musanja na Nyamrandirira UMEFANYIKA na MAOMBI ya Fedha za utekelezaji wa Miradi ya usambazaji wa MAJI Vijijini humo YAMEFIKISHWA Serikalini na yanafuatiliwa kwa ukaribu sana.