PROF MUHONGO AKAMILISHA AHADI YAKE YA SARUJI MIFUKO 100

Msaidizi wa Mbunge, Ndugu Fedson Masawa akikabidhi SARUJI MIFUKO 50

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo, Septemba 20, 2019 alikamilisha AHADI yake ya kuchangia SARUJI MIFUKO 100 kwa ajili ya Ujenzi wa Sekondari Mpya ya Kigera inayojengwa na Vijiji viwili vya Kigera Etuma na Kakisheri vyote vya Kata ya Nyakatende.
AHADI hiyo imekamilika baada ya Msaidizi wa Mbunge, Ndugu Fedson Masawa kukabidhi Kamati ya Ujenzi wa Sekondari hiyo SARUJI MIFUKO 50 kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo.
Kwa hiyo, idadi hiyo inakamilisha jumla ya SARUJI MIFUKO 100. Hapo awali, Mbunge wa Jimbo alikabidhi SARUJI MIFUKO 50 alipotembelea Kijiji cha Kigera Etuma na  kukagua Mradi huo wa Ujenzi.
Sekondari hii ikikamilika, Kata ya Nyakatende itakuwa na Jumla ya SEKONDARI 2 za Kata.
Akizungumza mara baada ya kupokea Saruji hiyo, Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Kigera Etuma, Ndugu Charles Manyonyi, akiongea kwa niaba ya Wananchi wa Vijiji vya Kigera Etuma na Kakisheri, amemshukuru sana Mbunge wa Jimbo lao, Prof Muhongo kwa MICHANGO yake MIKUBWA anayoitoa Kijijini hapo na ndani ya Jimbo zima la Musoma Vijijini.
Katibu wa Kamati ya Ujenzi wa Sekondari ya Kigera, Ndugu James Majengo amesema Wananchi wa Kigera Etuma na Kakisheri wataendelea na ujenzi kwa kasi kubwa ili kuhakikisha  Sekondari hiyo inafunguliwa January 2020.