KUANZA KWA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA LAMI YA MUSOMA-MAKOJO- BUSEKELA

kazi zinazoendelea kwenye ujenzi wa Barabara ya LAMI ya Musoma-Makojo-Busekela

AHADI ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli yaanza kutekelezwa kwenye Jimbo la Musoma Vijijini. Mhe Rais alitoa AHADI hii wakati wa Kampeni za UCHAGUZI wa 2015 akiwa Kijijini Kabegi, Kata ya Ifulifu.
BARABARA ya Musoma-Makojo-Busekela yenye urefu wa kilomita 92 imeanza KUJENGWA kwa kiwango cha LAMI. Ujenzi umeanzia kwenye LOT II (Kusenyi-Makojo -Busekela). LOT I ni Musoma-Mugango-Kusenyi.
Kuanza kwa MRADI wa ujenzi wa Barabara hii muhimu sana kwa UCHUMI na MAENDELEO ya Wilaya ya Musoma ni kielelezo na kithibitisho kingine cha MAFANIKIO ya UTEKELEZAJI wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020 ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374 linajishughulisha na KILIMO (mazao makuu: mihogo, mahindi, mpunga, viazi vitamu, matunda, mbogamboga,  pamba na alizeti), UVUVI (sangara, sato, dagaa, n.k.), UFUGAJI (ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku) na UCHIMBAJI MADINI (dhahabu).
Kwa hiyo BIDHAA za aina mbalimbali za kutoka Musoma Vijijini zitafika kwa uharaka na ubora wake kwenye MASOKO tarajiwa.
WANANCHI na VIONGOZI wa Wilaya ya Musoma yenye Jimbo la Musoma Vijijini WANAENDELEA kutoa SHUKRANI zao za DHATI kwa Mhe Rais wao, Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kutimiza AHADI aliyoitoa Jimboni mwao – ujenzi wa barabara ya LAMI.