WANAVIJIJI WA KATA YA BULINGA WAKUBALI KUTATUA TATIZO LA MRUNDIKANO WA WANAFUNZI MADARASANI

MKUTANO wa Mbunge Jimbo, Prof Sospeter Muhongo na WANANCHI wa Kata ya Bulinga.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
WANAFUNZI 157 wa Kata ya Bulinga wamechaguliwa kuendelea na MASOMO ya KIDATO cha KWANZA kwenye Sekondari ya Kata yao, yaani Bulinga Secondary School.
Hadi sasa, WANAFUNZI takribani 120 WAMERIPOTI Shuleni na wote WAMERUNDIKANA kwenye Chumba kimoja cha Darasa.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alitembelea Bulinga Sekondari na KUONGEA na WANANCHI akiwashawishi WASHIRIKIANE na SERIKALI yao kutatua TATIZO la UKOSEFU na UPUNGUFU wa Vyumba vya Madarasa kwenye Sekondari hiyo yenye Jumla ya WANAFUNZI 410.
Mwalimu Mkuu wa Bulinga Sekondari, Mwl Nyang’oso Chacha alisema Wanafunzi 157 wa Form I wanahitaji VYUMBA 3 VIPYA vya MADARASA na kwa sasa lipo BOMA la DARASA 1 liloezekwa tayari na linahitaji kukamilishwa. MABOMA 2 ya Vyumba 2 vya Madarasa hayajaezekwa.
Diwani wa Kata hiyo, Mhe Mambo Japan (CHADEMA) na Mwenyekiti  wa Serikali ya Kijiji cha Busungu, Ndugu Abel Mafuru (CCM) wamesema WANANCHI WAMEKUBALI kutoa NGUVUKAZI na KUCHANGA Shillingi 11,000/= kwa KILA KAYA ili KUKAMILISHA UJENZI wa VYUMBA 3 hivyo.
Aidha, Wananchi na Viongozi wa Kata ya Bulinga wanamshukuru sana Mbunge wao, Profesa Sospeter Muhongo kwa kushiriki na kuhamasisha shughuli za maendeleo kwenye Sekta ya Elimu na nyinginezo kwenye VIJIJI VYAO 3 – Bulinga, Bujaga na Busungu. Mbunge huyo alishachangia VITABU vingi, SARUJI MIFUKO 120 na MFUKO wa JIMBO ulishachangia MABATI 108.
UKAMILISHAJI WA VYUMBA 3 VIPYA VYA MADARASA
Wananchi wa Vijiji vyote 3 na Viongozi wao WAMEKUBALIANA kukamilisha ujenzi wa Vyumba hivyo 3 ifikapo tarehe 15 FEBRUARI 2020.
Kwa uharaka wa kupatikana CHUMBA cha PILI cha Form I ifikapo Jumatatu, 27.1.2020, Mbunge wa Jimbo amechangia, juzi (21.1.2020) SARUJI MIFUKO 35 ya kupiga lipu chumba kilichokwisha uzekwa.