WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kushirikiana na SERIKALI yao kutekeleza, kwa MAFANIKIO makubwa, MAAZIMIO yaliyowekwa kwa ajili ya kuinua kiwango cha ELIMU Mkoani Mara. MAAZIMIO hayo ni:
(1) Uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU ya aina zote katika Shule za Msingi na Sekondari.
(2) Kudhibiti UTORO wa WANAFUNZI kwa kuweka utaratibu wa KISHERIA wa kuthibiti tatizo hilo.
(3) Utoaji wa huduma ya CHAKULA cha MCHANA Shuleni (Msingi na Sekondari) ni LAZIMA. WAZAZI na JAMII nzima ya Mkoa wa Mara watengenezewe utaratibu wa kuchangia CHAKULA katika SHULE zao.
(4) Kuimarisha MAHUSIANO ya WALIMU na JAMII na NIDHAMU ya WANAFUNZI.
(5) Kudhibiti MIMBA kwa WATOTO wa KIKE na UKATILI wa WANAFUNZI.
(6) Kuimarisha USHIRIKI na USHIRIKISHWAJI wa JAMII katika MAENDELEO ya SHULE.
MSIMAMIZI MKUU wa utekelezaji wa MAAZIMIO hayo ni Mkuu wa Mkoa, Ndugu Adam Malima. akisaidiwa na Wakuu wa Wilaya zote na Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri zote.
JIMBO la Musoma Vijijini LINABORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU kwenye SHULE ZAKE ZOTE ambazo ni:
* SHULE ZA MSINGI 114 (111 za Serikali na 3 za Binafsi), na SHULE SHIKIZI 11 (nyingine bado zinajengwa)
* SEKONDARI 22 (20 za Serikali/Kata na 2 za Binafsi) na 5 MPYA zinazojengwa na zitafunguliwa mwakani (Januari 2021).
SAMANI ZA DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL
Sekondari hii ni MPYA iliyofunguliwa Januari 2020. WANANCHI wa Kata ya Bugoji wanaendelea na ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa, Maabara, Ofisi na Nyumba za Walimu.
SAMANI za Sekondari hiyo zinatengenezwa kwa MICHANGO kutoka kwa WANAVIJIJI na MBUNGE wao wa Jimbo.
UJENZI WA SHULE SHIKIZI
Shule SHIKIZI 11 kwenye VIJIJI 11 zinajengwa na kupanuliwa ziwe SHULE ZA MSINGI kamili zinazojitegemea. MALENGO MAKUU ya ujenzi huu ni kutokomeza MIRUNDIKANO Madarasani na UMBALI MREFU wa kutembea kwa Wanafunzi.
TAARIFA ya REDIO iliyoambatanishwa hapa inajitosheleza kwa maelezo.
SHUKRANI kwa VIKUNDI VYA PCI na WATAYARISHAJI wa Sherehe za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI kwa kuendelea KUHAMASISHA na KUCHANGIA upatikanaji wa CHAKULA kwenye SHULE za MSINGI na SEKONDARI za Jimbo la Musoma Vijijini.
TATHMINI YA KWANZA ya UTEKELEZAJI wa MAAZIMIO hayo itafanyika tarehe 30 AGOSTI 2020 chini ya Uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Mara.