Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SHULE YA MSINGI MKAPA ilianzishwa Mwaka 2009 na iko Kijijini Kastam, Kata ya Bukima.
Mwalimu Mkuu wake, Mwl
Nyakusanja David Mkangara amesema Shule hiyo ina jumla ya WANAFUNZI 972. Vyumba vya Madarasa VILIVYOPO ni nane (8) na UPUNGUFU ni kumi na nne (14).
Mwalimu Mkuu huyo anasema, “Hawapo Wanafunzi WANAOSOMEA NJE chini ya MITI lakini kuna MIRUNDIKANO MIKUBWA Madarasani ambapo Chumba kimoja cha Darasa chenye WANAFUNZI WENGI kinao 204 (Std III) na chenye WACHACHE kinao 87 (Std VI).”
TATIZO LA MIRUNDIKANO mikubwa Madarasani LINATATULIWA kwa KUJENGA Vyumba Vipya vya Madarasa.
Ndugu Adonias Matijo, Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Kastam amesema kuwa Kijiji hicho kilipokea Tsh 2,030,000/= ambayo ni RUZUKU (20%) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Fedha hizo zilitumika KUNUNUA SARUJI na kuanza kufyatua MATOFALI ya ujenzi wa Vyumba Vipya vya Madarasa.
Mbali ya FEDHA kutoka kwenye HALMASHAURI yao, KILA KAYA ya Kijiji cha Kastam inachangia NGUVUKAZI na FEDHA Taslimu ya kiasi cha Tsh 6,200/=
VYANZO hivyo vya FEDHA na NGUVUKAZI vimefanya WANAKIJIJI kufanikiwa KUJENGA Vyumba viwili (2) vya Madarasa na Ofisi moja (1) ya Walimu.
KAZI BADO KUBWA, Wanakijiji hao wanaomba WADAU wa Maendeleo na WAZALIWA na Kijiji cha Kastam na Kata ya Bukima kwa ujumla, WAJITOKEZE KUCHANGIA ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa ya S/M MKAPA. HARAMBEE ya Mbunge wa Jimbo itafanyika hivi karibuni.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO KWENYE S/M MKAPA
Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameishachangia:
* Madawati 160
* Vitabu vingi vya Maktaba
* Saruji Mifuko 60
* Mabati 54
MICHANGO YA MFUKO WA JIMBO KWENYE S/M MKAPA
* Saruji Mifuko 50
* Mabati 54
Diwani wa Kata hiyo (Bukima), Mhe January Simula amesema kwamba KATA YAO imejipanga kuhakikisha kwamba WANAFUNZI wa SHULE zote za MSINGI ndani ya Kata yao HAWATASOMEA NJE CHINI YA MITI ifikapo mwakani (Januari 2021).
Diwani huyo anawashukuru Viongozi wa Wilaya na Halmashauri yao, na Mbunge wao wa Jimbo kwa MICHANGO wanayoitoa kwenye MIRADI ya MAENDELEO (Elimu, Afya, Kilimo, Mazingira, Michezo, n.k.) ya Kata yao yenye VIJIJI 3 (Bukima, Butata na Kastam).
JIMBO la Musoma Vijijini LINAJENGA na KUBORESHA MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye SHULE zake zote za MSINGI 114 (111 za Serikali na 3 za Binafsi), SHULE SHIKIZI 11 (kati ya hizi zipo zilizofunguliwa).
Jimbo hili lenye KATA 21 na VIJIJI 68 lina SEKONDARI 22 zenye Wanafunzi (20 za Serikali/Kata na 2 za Binafsi). Sekondari MPYA 5 zinajengwa na zitafunguliwa mwakani (Januari 2021).