MATATIZO SUGU YA MIRUNDIKANO MADARASANI NA UMBALI MREFU WA KUTEMBEA YAENDELEA KUTATULIWA MUSOMA VIJIJINI

Ujenzi wa SEKA SEKONDARI ya Kata ya Nyamrandirira. Hii ni Sekondari ya pili ya Kata hiyo.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
JIMBO la Musoma Vijijini na HALMASHAURI yake (Musoma DC) linaendelea kutatua MATATIZO SUGU ya Mirundikano Madarasani na Umbali mrefu wa kutembea kwa WANAFUNZI na WALIMU. Utatuzi huu unafanywa kwenye SHULE zote za Msingi na Sekondari.
SEKONDARI ZILIZOPO
*Sekondari 20 za Serikali/Kata
*Sekondari 2 za Binafsi
*Sekondari MPYA zinazojengwa na ZITAFUNGULIWA Januari 2021ni:
(i) Kigera (inajengwa na Vijiji vya Kakisheri na Kigera, Kata ya Nyakatende – Sekondari ya PILI ya Kata)
(ii) Nyasaungu (inajengwa na Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifu – Sekondari ya KWANZA ya Kata)
(iii) Ifulifu (inajengwa na Kijiji cha Kabegi, Kata ya Ifulifu – Sekondari ya PILI ya Kata)
(iv) Nyegina (inajengwa na Vijiji vyote 3 vya Kata ya Nyegina – Sekondari ya PILI ya Kata), na
(v) Seka (inajengwa na Vijiji vyote 5 vya Kata ya Nyamrandirira – Sekondari ya PILI ya Kata)
Kwa hiyo ifikapo Januari 2021, JIMBO la Musoma Vijijini lenye Kata 21 na Vijiji 68 litakuwa na:
(i) SEKONDARI 25 za Serikali/Kata
(ii) SEKONDARI 2 za Binafsi
UJENZI WA KUSHIRIKISHA WANANCHI
Ujenzi wa SEKONDARI hizo MPYA unaendeshwa kwa USHIRIKIANO wa: SERIKALI na HALMASHAURI yake (Musoma DC), WANAVIJIJI, MBUNGE wa JIMBO, WAZALIWA (baadhi) wa KATA zinazojenga na WADAU wengine wa MAENDELEO.
UJENZI WA SEKONDARI MPYA KIJIJINI SEKA
WANANCHI wa Kata ya Nyamrandirira yenye VIJIJI 5 (Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka) IMEAMUA KUJENGA SEKONDARI YA PILI ili kutatua MIRUNDIKANO iliyopo Kasoma Sekondari. Vilevile, SEKA SEKONDARI ITAPUNGUMZA UMBALI wa kutembea kwa WANAFUNZI wa kutoka VIJIJI vya Seka, Mikuyu na Chumwi.
AFISA MTENDAJI wa Kata ya Nyamrandirira, Ndugu Muswaga Itra, amesema kwamba WANANCHI ndani ya VIJIJI vyote 5 wanachangia NGUVUKAZI na FEDHA taslimu ambazo zimeamuliwa na VIJIJI vyenyewe (kati ya Tsh 20,000 na 5,000 kutoka kila KAYA).
MICHANGO mingine imetolewa na MGODI wa SEKA ikiwa ni TRIPU 23 za MAWE na TRIPU 1 ya MCHANGA.
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameishachangia SARUJI MIFUKO 250.
DIWANI wa Kata hiyo, Mhe Obadia Maregesi amesema kwamba kwa sasa UJENZI ni wa MASHINDANO kati ya VIJIJI vyote vitano (5) na amesisitiza kwamba UJENZI wa VYUMBA 8 vya Madarasa ya Sekondari hiyo vitakamilika hivi karibu na MIUNDOMBINU mingine muhimu itakamilika kabla ya tarehe 30 Septemba 2020.
OMBI KUTOKA VIJIJINI
WANANCHI wanawaomba sana WAZALIWA wa VIJIJI 5 vya Kata yao WAJITOKEZE KUCHANGIA UJENZI huu.